Jumatatu, 5 Februari 2018

Mwalimu Oscar Samba Kitabu cha NAMNA YA KUTOKA KWENYE KIFUNGO AU HALI YA KUKATALIWA.


Leo ninakuletea tu Utangulizi wake, na niyangu rai kukutaka kufuatilia kitabu hiki punde kikiingia Sokoni, pia kwa dhati kabisa ninaomba maombi yako ili nikikamilishe vyema na tena kwa wakati.
Utangulizi:Utangulizi:


Kukataliwa maana yake ni kukosa kibali. Hali inayokufanya kukosa mvuto mbele ya wahusika, kutokudhaminika, au kuwa na dhamani ama sifa ama kupata heshima stahiki kutoka kwa jamii inayokukataa ama kukubagua.
Kuna vitu watavifanya bila kukushirikisha angali ulistaili kufanyiwa hivyo, ukisoma kisa kile cha kupakwa mafuta kwa Daudi, utaona kuwa watoto wengine wote waliitwa ila Daudi pekee hakuitwa kwani alisaulika;
1 Samweli 16: 10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Tatizo la kukataliwa huwalinaumiza, linajeruhi, na kumuacha muhisika akiwa katika hali ya unyoge, na kukosa raha, na hali hiyo hiyo ya maumivu ispopata tiba ya haraka huweza kusababisha madhara makubwa mno katika kiroho cha mtu na kimaisha kwa ujumla.

Jumamosi, 3 Februari 2018

Pata Dondoo za KITABU UCHUMBA SALAMA KATIKA KRISTO YESU Katika mada ya Namna ya Kuishi Salama Maisha ya Uchumba hadi Ndoa. Utajionea Hatua Muhimu za Kuchukua, Ikiwemo ya Kuchagua Mshenga Wajibu wake, Madili na Wasifu wake:

Namna ya Kuishi Salama Maisha ya Uchumba hadi Ndoa.
Kusudio la mada hii ni kukuwezesha kuishi vyema kiroho na kimwili, au kiushuhuda katika maisha ya uchumba.
Swala la ushuhuda ni muhimu sana katika hatua hii maana litawajengea heshima, kwa jamii, jamaa wako wa karibu kiundugu na kanisa kiujumla, kwa hiyo ipo haja ya kuwa salama kiroho na kimtazamo au machoni pa watu pia.
Maana ni vizuri kuhesabiwa haki na Mungu lakini pia wanadamu wakuheshimu. Maana hali hii itakupa haki kwao, lakini pia itaifanya huduma yako kukubalika, maana katika ulimwengu huu tunamuhitaji Mungu kweli ili tufanikiwe, lakini pia tunawahitaji wanadamu, na wanadamu hutazama kwa macho ya kimwili ili kuona, sio ya moyoni na nje kama Mungu.
Maana yangu hapa ni kukutaka kuepukana na mitazamo finyu ya vijana kadha kuwa anaishi kama vile atakavyo yeye madamu hatendi dhambi kwake sio mbaya.
Na kujaribu kutengeneza mazingira ya ushuhuda kwake ni unafiki, huku ni kukosa maarifa.
Hali ya kupita kila kona, au kukaa ovyo na mwenzako ama kukutana katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa mboni za wanadamu, kwa madai kuwa nyie mpo vema kiroho hata kama hamtendi kosa la kukutana kimwili, lakini pia kufanya hivyo ni dhambi.
Inaweza isiwe na madhara au matokeo kama vile ya kujamiiana, ila hali ya kuharibu ushuhuda kwa makusudi ni kosa kiroho.
Paulo Mtume anasema sisi ni barua, licha ya hivyo, anatuambia kama akila nyama itamkwaza jirani yake, yupo tayari kutokuila, unaweza kujione uchaji wa mtumishi huyu ulivyokuwa mkubwa.
Kwa hiyo nawe unawajibika kujiwekea mazingira salama ili jina la Bwana lisitukanwe, hali ya kusema kuwa Mungu anatizama moyo, au ya kuku mayai na ya watu maneno, eti huwezi kuwazuilia kunena, unapaswa kuwa makini ili kumtetea Kristo.
“Madamu sitazini, si dhambi mtumishi.” Acha ujinga, linda ushuhuda.
Huduma nyingi za watu zimekufa, kwa kukosa hii hekima, zimeishilia kupakwa matope na uvundo wa kila namna.                      Karibu:
(a) Jinsi ya Kutenda Vyema.
(i) Zifahamu Sheria au kanuni za Kanisani kwako, makanisa mbalimbali yametofautia kivigezo, yapo ambayo ili ufunge ndoa au hata uchumba kutangazwa ni lazima, muhusika awe anaudhuria ibada za Ushemasi, Seli, au Jumuia, wenine huziita ibada za Nyumbani, au Kanisa la nyumbani.
Hususani makanisa makubwa huwa na sera hii ili kuweza kuwa na taarifa sahihi za mtu anayenuia kuchukuwa hatua hiyo, kwani kama kanisa lina watu wengi ni vigumu kwa uongozi wa kanisa la mahali pamoja, kujua tabia zake, na kama kweli ana vigezo na sifa za kufikia hatua hiyo, maana wengine huweza kuwa na ndoa nyingine au alishawai kuolewa, na muda wake katika wokovu, na pia hali yake ya kiroho.
Kwa mantiki hiyo, kikundi cha ibada za Jumuia, huweza kukufahamu vizuri zaidi.
Lakini pia wengine, ni shariti uwe umelipa au kutoa Zaka ama fungu la kumi, kwa kipindi kisicho pungua miezi 6.
Pia vigezo vya muda wako wa wokovu au kuabudu hapo kanisani ni muhimu sana.
Kufahamu kanuni na taratibu kama hizo, kutakusaidia kutokuingia katika malumbano ya kihoja na wahusika, pia kutakuokolea muda, licha ya kukuokolea muda kutakufanya kutenda vyema.
Maana nimewaona watu walioabudu makanisani muda wa miaka mingi lakini kwa kuwa walipohamia walihamia kienyeji, yaani bila barua ya utambulisho, walijikuta wakizuiliwa, kuchuku hatua hizi za Uchumba hadi ndoa, na swala lipo sana kwenye huduma zenye watu wengi.
Hatua za Kuchukuwa mkishakubaliana:
(ii) Nendeni kwa Mchungaji, kama mna abudu katika makanisa tofauti tofauti, ni vyema mkaanza katika kanisa la kijana wa kiume, au tumieni utaratibu kwa kila muhusika kumuendea mchungaji wake, na mara baada ya hapo ndipo muwaende walezi wate. Ila kibusara anzeni kwa wakiume.
Ili kulinda ushuhuda mnaweza kuamua kukutana kanisani, ama kutumia utaratibu wa kuambatana na washenga au mshenga.
 (iii) Tafuta Mshenga na uambatane nae, ni muhimu kuanza kutafuta mtu huyu maana atafanyika msaada mkubwa kwako, kama utatambua nafasi yake vyema.
Lakini mara baada ya kumpa, huna budi kuhakikisha kuwa unambatana nae, ili kutimiza adhima na dhima ya uwepo wake.
Sifa za Mshenga:
(1) Awe Mchamungu, sifa hii ni muhimu ili aweze kukubeba rohoni, na kukushauri kiroho, lakini pia aweze kukulinda vyema kiroho, pia asije kuhusika katika kukushawishi kuingia majaribuni, pia ili kumrahishia Mungu pale atakapotaka kufikisha jambo fulani kwenu aidha kwa njia ya mashauri na mahusia kutoka kwake.
(2) Awe na uelewa wa kutosha kuhusu Mambo haya, Anapaswa kuyafahamu kwa kiasi fulani maswala ya uchumba, ili aweze kukaa vyema kwenye nafasi yake.
(3) Awe na Uwezo wa Kukushauri na Ujasiri wa Kukukemea, Ajawe na Hekima lakini pia Busara, ili kukusaidia katika kuchukuwa maamuzi fulani, maana kuna majira mambo huweza kuwa magumu kiutatuzi, ila hekima yake na Busara zake huweza kutumika katika kuleta

Alhamisi, 14 Desemba 2017

Kitabu cha NAMNA YA KUTOKA KWENYE KIFUNGO AU HALI YA KUKATALIWA.

Leo ninakuletea tu Utangulizi wake, na niyangu rai kukutaka kufuatilia kitabu hiki punde kikiingia Sokoni, pia kwa dhati kabisa ninaomba maombi yako ili nikikamilishe vyema na tena kwa wakati.
Utangulizi:
Kukataliwa maana yake ni kukosa kibali. Hali inayokufanya kukosa mvuto mbele ya wahusika, kutokudhaminika, au kuwa na dhamani ama sifa ama kupata heshima stahiki kutoka kwa jamii inayokukataa ama kukubagua.
Kuna vitu watavifanya bila kukushirikisha angali ulistaili kufanyiwa hivyo, ukisoma kisa kile cha kupakwa mafuta kwa Daudi, utaona kuwa watoto wengine wote waliitwa ila Daudi pekee hakuitwa kwani alisaulika;
1 Samweli 16: 10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. 
11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. 
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Tatizo la kukataliwa huwalinaumiza, linajeruhi, na kumuacha muhisika akiwa katika hali ya unyoge, na kukosa raha, na hali hiyo hiyo ya maumivu ispopata tiba ya haraka huweza kusababisha madhara makubwa mno katika kiroho cha mtu na kimaisha kwa ujumla.
Daudi ni miongoni mwa watumishi walikumbwa na hali au na kadhia hii kwenye Biblia, pia imo kwa Musa, Musa alitaka kuwakomboa wana wa Israeli maana mmoja wao alipoonewa na Mmisiri alihakikisha anamuwa yule muonevu, na alipowaona wao kwa wao wanapigana alijaribu kuwapatanisha, lakini yule muonevu alimgeukia na kuibua hali ya kumkataa Musa kama muamuzi, jambo lililochangia kutoroka au kuikimbia ile nchi, ingawaje sababu nyingine ni hofu kwa Farao, ila na hii ilichangia, maana hakuwa na makazi tena yaliyosalama, kwa Wamisiri Farao anawinda roho yake, na kwa Waebrania wenzake, hawamtaki.

NAFASI YA NVUVU ZA KIROHO KATIKA KUKUTAJIRISHA, KWA WAFANYA BIASHARA NA WASANII. Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha NAFASI YA ULIMWENGU WA ROHO TAKIKA UONGOZI, (kiti cha Enzi)

Image may contain: 2 people, people standing and suit
Mwalimu Oscar Samba na Mtume Doggy Lasi wa nchini Kenya wakiwa katika picha ya Pamoja, Picha na Makitaba yetu.
.
Kwenye Biashara:
Biashara inaweza isiingie moja kwa moja katika kundi la uongozi ila zipo zilizoinuka nakufikia hatua ya kampuni  au taasisi fulani ambazo zina mfumo wa uongozi ndani yake, pia Migahawa na hata Hoteli, Shule na vikundi fulani vya ujasiriamali na kiuchumi ni miongoni mwavyo.
Lakini hapa ninazungumzia biashara kwa ujumla bila kujali kubwa au ndogo, maana shuhuli yoyote ile ya kiuchumi inayofanywa na mtu ni lazima iwe na nguvu ya ulimwengu wa roho.
Ndio maana yapo makabila fulani biashara au kazi ikienda mrama hupiga simu nyumbani ili warekebishe mambo, pia wengine kila mwezi fulani hukutanyika nyumbani kwa ajili ya ibada za mizimu, hapo huchinja ama kufanya mila na wazee kuwaombea dua fulani.
Hilo ni kundi la kwanza, la pili ni lile ambalo kuna wazee au viongozi wao wa kidini na kuomba dua kutoka kwao, wengine huwapungia mapepo maalumu ya biashara au kuwaombea kwa mungu ama mzimu wanao uabudu.
Kundi jingine la tatu ni wale wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au wasoma nyota, ama wachawi, ama kufanya ushirikina wowote ule.
Kundi la nne ni wale wanaomuabudu Shetani moja kwa moja, yaani hawa wanafahamu kabisa kuwa wanamuabudu na kumtumikia Lusifa, dini yao huitwa ya Mashetani, Kikundi cha “Freemason” na vinginevyo ni miongoni mwavyo.
Wanachama wake au walio wengi huingia huko ili wapate fedha, mvuto kwenye usanii kama wana muziki, waigizaji, au kibali kwenye siasa na kwa bahati mbaya hata viongozi wa kidini nao wamejipenyeza kwenye makundi hayo, kuna alingine pia wanaliita, “Iluminate.”
Makundi yote hayo niliyoyataja yanatafuta nguvu za kiroho katika biashara kutoka kwa Shetani, sababu ya wafanya biashara kufanya hivyo ni kutokana na uhalisia kuwa swala la biashara hufanyika kiroho ama ili kuweza kufanya biashara mwilini ama kuwa na uwezo wa kumiliki na kutawala kiuchumi ni lazima uwe na nguvu za ulimwengu wa roho, ambazo hupatika aidha kwa Yesu au Shetani, sasa wasio na Yesu, hulazimika kutumia njia za mkato. Nakupa andiko linalodhibitisha jambo hili:
Ufunuo 17-19. (17:4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

17:5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.)
Jina lake ni, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI, Ndiye yule anayewapa wanasiasa nguvu ya kutawala, pia ukisoma kwa umakini Sura ya 17-19 ya Ufunuo utafahamu kuwa maandiko yanasema kuwa wametajirishwa kwa kiburi chake;
 (Ufunuo 18:3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.)
Nakumegea hii siri: Kumbuka hilo andiko linasema kuwa wafalme, ukiona wafalme fahamu ni wanasiasa au viongozi wa uongozi wa dunia hii, pia wafanya biashara, alafu wamepata mali au uongozi kwa kiburi chake, ndio maana mwanasiasa anapoingia madarakani anakuwa na kiburi sana, wapo tayari watu wauwawe, ila wao waendelee kutawala, wapo tayari kuziona damu za watu wasio na hatia zikimwagika lakini ulaji wao usipunguke, alikadhalika wafanya biashara, mara baada ya kuipata mali huingiwa na roho ya kiburi, ukiyaona hayo usishangae fahamu kiti kinachowawezesha au nguvu inayowanufaisha ama kuwafanikisha ndiyo inayoachilia hiyo roho ya kiburi, ndipo ninasema kuwa udhamini wa ulimwengu wa roho unaotoka kwa Yesu una dhamani kubwa sana. (Tusonge mbele na Biashara)

Jumatatu, 6 Novemba 2017

HUDUMA YA MWALIMU OSCAR VITABU NI JIBU LA KUDUMU KIROHO, KINDOA, KIUCHUMI NA HATA KISIASA NA KIJAMII.

Huduma ya MWALIMU OSCAR VITABU, Imebainisha kuwa imebeba majibu mengi ya maswali na mambo magumu yanayoikabili jamii siku ya leo ikiwemo ile ya Kikristo na isiyo ya Kikirsto.

Hayo yamebainishwa jana (5/11/2017) na Mkurugenzi Mkuu wa huduma hii Mwalimu Oscar Samba wakati akitoa risala kwa mgeni Rasimi katika siku ya Uzinduzi wa vitabu vya USIFIE JANGWNAI na cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.

Mwalimu alielezea maono na malengo ya huduma hii mambo ambayo yanalenga kutoa majibu au kufanyika msaada mkubwa kwa jamii katika utatuzi wa maswala mablimbali yanayoikabili.

Kwa hivi sasa jamii inakabiliwa sana na tatizo la kutokumjua Mungu, kuduma kiroho, Migogoro kwenye ndoa, na hata zile zilizo salama kiamani, nyingi, bado hazitimizi vyema  kusudi kuu la kuwekwa kwake na Mungu.

Pia lipo tatizo la kiuchumi, kwani wana wengi wa Mungu wamekuwa wakiishi maisha  magumu, pamoja na wale wa dunia hii.

Jambo jingine ni kutokuwa na viongozi sahihi au wenye kuwajibika ipaswavyo, wale wakiroho yaani Watumishi, na wakijamii na serikali yaani wanasiasa.

Pia jamii inakabiliwa na tatizo la uzito kifikra, na hii inatokana na kutokuwepo kwa mahubiri, mafundisho na maarifa yanayolenga kuleta ukombozi.

Mambo yote hayo yamo katika kusudi la huduma hii, nami ninakuletea Maono na Malengo pamoja na Mafaniko, sanjari na Changamoto ya huduma hii kama ilivyoelezwa hapo jana na Mkurugenzi.

Maono: Kuwa na jamii salama kiroho na kifikra yenye mafanikio ya kimwili na kiroho katika nyanja muhimu kama ya kiuchumi, kisiasa, na kuwa huru kiroho katika Kristo Yesu.
Malengo makuu  ya Huduma: 1. Kuikomboa jamii kiroho, kiuchumi, na kisiasa. 2. Kuzifanya ndoa kuwa sehemu salama, ili kufanikisha kusudi lake vyema. 3. Kuandaa viongozi wazuri na wawajibikaji kiroho. 4. Kujenga umoja katika Mwili wa Kristo.
Pia 5. Kuwa na Gazeti la kila wiki, na 6. Kutoa Jarida kila baada ya miezi, 7. Pamoja na kuwa na Press yetu wenyenye kwa ajili ya kuprinti vitabu. Itakayoitwa, Haleluya Press.
Mafanikio: 1. Kuandika vitabu Takiribani 24, ikiwemo 12 vya familia na ndoa, pia vipo vyenye dhima ya kiuongozi kiroho, mfano cha HEKIMA YA KIUONGOZI KIHUDUMA. Pia 2. Kufanikiwa kuvitoa vitabu viwili ambavo leo ndio vinazinduliwa.
Changamoto: Ndugu Mgeni Rasimi, zipo changamoto kadhaa ambazo zinatukabili, hakika zikitatuliwa huduma hii itafanya kazi katika ufanisi mkubwa sana.
1. Upungufu wa vifaa vya kuandikia na uchapaji pia uandaaji wa vitabu , tunahitaji Komputa moja ana ya Desktop, yenye dhamani ya shilingi 500, 000/=, kwa ajili ya kuandikia, Printer ya Epsoni yenye dhamani ya sh 650, 000/=.
2.  Mtaji kwa ajili ya Kuprinti vitabu, Ndugu mgeni rasimi, huduma hii imeanza katika nyakati ngumu sana kiuchumi, hadi sasa kazi hii tumeifanya kwa imani kubwa, hapa tulipo tuna deni la zaidi ya sh 300, 000/=.
Ili kuweza kufanya kazi hii kwa wakati na ufanisi mkubwa, tunahitaji walau mfuko wetu uwe na shilingi 600, 000/=.
3. Ukosefu wa Ofisi, Ndugu mgeni Rasimi huduma hii kama niivyokujuza hapo awali kuwa imeanza kiimani, kwani hadi hivi sasa hatuna ofisi kwa ajili ya shuhuli zetu, badala yake, nyumbani au chumbani kwa mkurugenzi Mkuu ndimo ilipo Ofisi, kama unavyojua mazingira ya nyumbani, na matumizi ya meza ya ofisi yanapoingiliana yale ya nyumbani, hali ambayo sio salama kihuduma au kiofisi.
Pia swala hili linazuilia wageni au watu wanao hitaji huduma kuipata kwa urahisi.

4. Ukosefu wa mawakala, Ndugu Mgeni rasimi ni yetu kiu kutuwezeha kupata mawakala wengi ili kurahisisha swala la usambazaji na uzaji wa vitabu hivi.

 Mungu akubariki na kama unahitaji vitavu vyetu tafadhali wasiliana nasi kwa namba nitapakayo kupa punde na pia ukitaka kutoa sadaka yako waweza itoa kupitia hiyo Namba: +255 75 985 9287

TAZAMA PICHA ZA UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA

Jana Huduma ya MWALIMU OSCAR SAMBA VITABU ilifanikiwa kuzindua vitabu viwili, ambavyo ni USIFIE JANGWANI na ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.

Na zifuatazo ni picha za tukio hilo:
Mkurugenzi wa huduma ya MWALIMU OSCAR VITABU, Mwalimu Osar Samba akinena jambo wakati wa kusoma risala kwa Mgeni Rsimi.

Jumamosi, 4 Novemba 2017

NI KESHO UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA, MGENI RASIMI NI EMANUELI SHILATU.

Kava la kitabu cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU
Kava la kitabu cha USFIE JANGWANI na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU
Huduma ya Uandishi wa Vitabu vya Kiroho ya MWALIMU OSCAR SAMBA kesho tarehe 5/11/2017 inatarajia kufanya uzinduzi wa vitabu vyake vipya viwiwli, cha USFIE JANGWANI na kile cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.

Akizungumza na blogu hii Mkurugenzi Mkuu Oscar Samba aliye pia mwandishi wa vitabu hivyo amesema kuwa mgeni rasimi anatarajiwa kuwa ni Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Binafi ya KING DAVID  na pia ni Mkurugenzi  wa huduma ya mafunzo ya mafanikio kiuchumi kupitia Biblia ya KINGDOM BUSINESS.

Afla hiyo ya uzinduzi inatarajiwa kufanyika katika kanisa la TAG VCC Lililopo katika eno la Morombo hapa Mkonia Arusha nchini Tanzania.