Alhamisi, 14 Desemba 2017

NAFASI YA NVUVU ZA KIROHO KATIKA KUKUTAJIRISHA, KWA WAFANYA BIASHARA NA WASANII. Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha NAFASI YA ULIMWENGU WA ROHO TAKIKA UONGOZI, (kiti cha Enzi)

Image may contain: 2 people, people standing and suit
Mwalimu Oscar Samba na Mtume Doggy Lasi wa nchini Kenya wakiwa katika picha ya Pamoja, Picha na Makitaba yetu.
.
Kwenye Biashara:
Biashara inaweza isiingie moja kwa moja katika kundi la uongozi ila zipo zilizoinuka nakufikia hatua ya kampuni  au taasisi fulani ambazo zina mfumo wa uongozi ndani yake, pia Migahawa na hata Hoteli, Shule na vikundi fulani vya ujasiriamali na kiuchumi ni miongoni mwavyo.
Lakini hapa ninazungumzia biashara kwa ujumla bila kujali kubwa au ndogo, maana shuhuli yoyote ile ya kiuchumi inayofanywa na mtu ni lazima iwe na nguvu ya ulimwengu wa roho.
Ndio maana yapo makabila fulani biashara au kazi ikienda mrama hupiga simu nyumbani ili warekebishe mambo, pia wengine kila mwezi fulani hukutanyika nyumbani kwa ajili ya ibada za mizimu, hapo huchinja ama kufanya mila na wazee kuwaombea dua fulani.
Hilo ni kundi la kwanza, la pili ni lile ambalo kuna wazee au viongozi wao wa kidini na kuomba dua kutoka kwao, wengine huwapungia mapepo maalumu ya biashara au kuwaombea kwa mungu ama mzimu wanao uabudu.
Kundi jingine la tatu ni wale wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au wasoma nyota, ama wachawi, ama kufanya ushirikina wowote ule.
Kundi la nne ni wale wanaomuabudu Shetani moja kwa moja, yaani hawa wanafahamu kabisa kuwa wanamuabudu na kumtumikia Lusifa, dini yao huitwa ya Mashetani, Kikundi cha “Freemason” na vinginevyo ni miongoni mwavyo.
Wanachama wake au walio wengi huingia huko ili wapate fedha, mvuto kwenye usanii kama wana muziki, waigizaji, au kibali kwenye siasa na kwa bahati mbaya hata viongozi wa kidini nao wamejipenyeza kwenye makundi hayo, kuna alingine pia wanaliita, “Iluminate.”
Makundi yote hayo niliyoyataja yanatafuta nguvu za kiroho katika biashara kutoka kwa Shetani, sababu ya wafanya biashara kufanya hivyo ni kutokana na uhalisia kuwa swala la biashara hufanyika kiroho ama ili kuweza kufanya biashara mwilini ama kuwa na uwezo wa kumiliki na kutawala kiuchumi ni lazima uwe na nguvu za ulimwengu wa roho, ambazo hupatika aidha kwa Yesu au Shetani, sasa wasio na Yesu, hulazimika kutumia njia za mkato. Nakupa andiko linalodhibitisha jambo hili:
Ufunuo 17-19. (17:4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

17:5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.)
Jina lake ni, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI, Ndiye yule anayewapa wanasiasa nguvu ya kutawala, pia ukisoma kwa umakini Sura ya 17-19 ya Ufunuo utafahamu kuwa maandiko yanasema kuwa wametajirishwa kwa kiburi chake;
 (Ufunuo 18:3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.)
Nakumegea hii siri: Kumbuka hilo andiko linasema kuwa wafalme, ukiona wafalme fahamu ni wanasiasa au viongozi wa uongozi wa dunia hii, pia wafanya biashara, alafu wamepata mali au uongozi kwa kiburi chake, ndio maana mwanasiasa anapoingia madarakani anakuwa na kiburi sana, wapo tayari watu wauwawe, ila wao waendelee kutawala, wapo tayari kuziona damu za watu wasio na hatia zikimwagika lakini ulaji wao usipunguke, alikadhalika wafanya biashara, mara baada ya kuipata mali huingiwa na roho ya kiburi, ukiyaona hayo usishangae fahamu kiti kinachowawezesha au nguvu inayowanufaisha ama kuwafanikisha ndiyo inayoachilia hiyo roho ya kiburi, ndipo ninasema kuwa udhamini wa ulimwengu wa roho unaotoka kwa Yesu una dhamani kubwa sana. (Tusonge mbele na Biashara)

Maandiko yanatuambia kuwa kuna majira yatakuja hususani kipindi cha dhiki kuu na Mungu atampiga huyu Pepo anayewatajirisha, na hakutakuwa na nguvu hii tena juu ya hao wafanya biashara hali itakayowafanya washindwe kuuza maana hakuna mnunuzi, andiko hili likupe kufahamu kuwa kumbe anayeenda kwa waganga, au kujiunga na makundi ya kishetani, ama kufaya mila au ibada kwa miungu ya kigeni ni ili apate nguvu za kuuza, ndiposa wewe unaweza ukawa unauza machungwa tena mazuri , na jirani yako anauza hayo hayo tena yamenyauka, ila watu hukuruka wewe na kwenda kwake, ukiona hivyo fahamu kuna nguvu anaitumia, ila mimi nimekuandikia haya ili kukufanya kuitafuta nguvu ya Yesu maana utajiri wake ni wakudumu, “Ok” Tulione hilo andiko la anguko la huyu Pepo:

Ufunuo wa Yohana 18:11 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;
18.12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari.
Ndiposa nguvu hizi zikichuja, huyu mtu huhakikisha anarudi kijijini kwao ili wazee wa mila wamuwekee mambo sawa, maana hakuna anayenunua tena vitu vyao, wengine hurudi kwa mganga, wengine hufanya maagizo fulani ikiwemo kafara.
Madhara ya kuitegemea nguvu ya Shetani ni mbaya sana, maana kanuni za Shetani ama mashariti yake huwa na maumivu makubwa mno, mfano, anakutaka kumtoa mwanao kafara, kumfanya ndondocha, kuchukuwa watu misukule, wengine wanalala makaburini, wapo wanaopewa maagizo ya kula maiti, hakika ni mateso makubwa mno.
Wapo ambao pia wanaopewa mashariti ya kutokulala ndani, wanalala porini, wengine hulala chini, wapo wanaolazimishwa kuvaa mavazi machafu au yasiyo nadhifu, kutokupada gari angali na magari, sasa fedha zisizokunufaisha wewe zina faida gani?
Baya zaidi ukifa leo unaenda Jehanum ya Moto, sasa kuna faida gani kuipata dunia yote na kisha kuingia hasara ya roho yako katika Jehanum ya moto milele?
Na ubaya wa huu utajiri ukishindwa mashariti unaweza ukafa, au kuwa kichaa, ama wenzako kukuchuku msukule ama kukufanya ndondocha mara baada ya kuchukuli kwa nyota yako ya mafanikio na kiufahamu, pia inaumiza pale unapozaa watoto na kumlisha pumba kishirikina ili tu upate mali, unaza mwana lakini unamfanya ndondocha ili tu upate fedha, kumbuka ukifa hizo damu za watu utadaiwa, najua unaweza usinielewe na ukapuzia kwa ajili ya kiburi, maana huyu Mama wa machafuko anayekutajirisha hufanya hivyo kwa kiburi chake, sasa nawe ni lazima kiwe juu yako, ila fahamu kuna siku utalia na kusaga meno katika Jehanum ya moto milele katika lile ziwa liwakalo moto.
Ndugu yangu kama umeingia huko geuka leo leo, ya mkini uliingia huko ili upate uongozi fulani, kumbuka Daudi na Yusufu walikuwa wanasiasa na walifanikiwa katika Kristo Yesu vyema tena sana, pia uwenda uliingia huko ili upate utajiri, maandiko yanatumbia kuwa kwa Yesu upo Utajiri, tena wenye heshima, sio utajiri tu bali ni Utajiri Udumuo, Utajiri wa Yesu hauchuji, ni wa kizazi hadi kizazi, Ibrahimu alimridhisha Isaka, kisha Yakobo, Yakobo Israeli na hadi leo mimi na yule aliyeokoka, ila utajiri wa kipepo ukishindwa mashariti unapuputika kama uyoga, utashangaa jana nyumba imeungua moto, kesho gari limepata ajali, na kesho kutwa fulani kafa, watakwambia ni Shindikizo la Damu lakini kiukweli ni  Shetani kachukua vuno lake, watasema ni shoti ya umeme ndio imesababisha ajali ya moto, au gari “lili-feli” breki ila kiuhalisia wenye mali yao wameichukua, wengi wakifa wanakufa na mali zao, ila waliokoka, hurithisha watoto wao, kama Ibrahimu na vizazi vyake vyote, sasa kama umeamua kuokoka tafadhali fungua ukurasi wa tatu kutoka mwisho wa kitabu hiki hapo ipo SALA YA TOBA, Ifuatishe kwa imani nawe utakuwa umeokoka.
Pia chonde chonde kama bado hujajiingiza katika harakati hizi za nguvu za kipepo ili kujipatia mali, ni yangu Rai kukutaka kuachana na njia hizo maana zitakukwamisha na kukupa maumivu mkubwa badala yake mtegemee Yesu.
Wanamuziki/ Waigizaji: Ni hatari sana kutegemea nguvu za kipepo katika kazi au vipawa mulivyopewa na Mungu, unapojiunga na vikundi vya kishetani kama “Freemason” maana yake ni kwamba mnamfanya Mungu aliyewapa hivyo vipawa amekosea kuwapa, pia mnampa Shetani mwanya wa kueneza roho zake chafu na mbaya kwenye jamii.
Mfano mapepo mahaba yamekuwa yakienezwa na miziki na maigizo yaliyokosa maadili, mavazi yako, kucheza kwao na maudhui ya nyimbo zao yamekuwa ni sehemu kubwa ya kumueneza huyu Pepo Mchafu.
Kumekuwa na matukio ya ajali kweye “Show” za wasanii, ikiwa ni njia ya mapepo kupokea kafara zao.
Yupo msanii mmoja wa maigizo hapa nchini ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama wa kukindi moja wapo hapo, alisema kuwa alipewa mapete ya kipepo huko na hao waabudi Shetani wenzake, ambapo ilikuwa akisinzia kwenye ngari na pete zikigongana tu lazima ajali itokee mahali, jaribu kufikiri!
Shetani anakutumia kama lango la kuwaangamiza au kumwaga damu isiyo na hatia, kwa sababu tu eti upate mvuto kwa watu, utajiri au umaarufu fulani.
Yesu aliyemuinu muimbji Daudi wa Zaburi, Sulemani mwanae aliyetutungia Mithali nzuri na Wimbo Ulio Bora, pamoja na Wana wa Asafu, hakika na wewe atakuinua, toka kwenye kuimba nyimbo za dunia hii na Okoka sasa ili uimbe nyimbo za Kristo Yesu, (Nyimbo za Injili).
UTAJIRI KUTOKA KWA YESU:
Sasa tuuone Utajiri unaotokana na nguvu za Mungu, na nitakupatia andiko linalodhibitisha kuwa Mungu anazo nguvu za kukupatia wewe huu utajiri, ili kukufanya kuachana na kutegemea zile za kishetani, ama kufikiri kufanya hivyo, kama ni umaarufu, ule wa Yesu ni kiboko, kama ni mvuto, hakuna mvuto mkubwa kama wa Yesu, ukitaka kuamini wewe kamulize Musa, Yusufu, na wengine akiwemo Daudi waliodharaulika ila walikuja kuwa watu waliokubalika na wenye kibali kikubwa sana. (Tugeukiye Utajiri Wa Ki-Yesu):
Kumbukumbu la Torati 8: 17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
Hilo andiko linatupa udhibitisho kuwa nguvu za kibinadamu haziwezi kuleta utajiri, ndiposa wasiomjua Mungu hutafuta zile za kipepo, lakini ajenda yangu ni kukutaka kuzitafuta za kimungu na nikulingana na faida zake, nami sitaki kuwa na hadithi nyingi bali ninakupa andiko la chini yake linalodhibitisha uweza wa Mungu kiutajiri;
Kumbukumbul la Torati 8: 18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Mungu anatudhibitishia kuwa anatoa nguvu za kupata utajiri, sasa tuuone au tuzione sifa za utajiri wake:
1. Unamashariti nafuu na yasiyo na madhara, kiafya, na kiroho, Mungu hakwambi kwamuwe ndugu yako, mfanye fulani kuwa ndondocha, au kale maiti, ama lala nje, bali hukuhitaji kumtolea sadaka katika fedha alizo kupa, ikiwemo Fungu la Kumi, na sadaka ya hiyari ya moyo wako, kukutaka kutokuiacha imani ya kiroho, ambapo hapo pia ni kwa faida yako, yaani anakutaka kupata fedha na mbinguni uende, Shetani hukutaka kupata fedha ya aibu, huku ndugu zako wakisalia kuwa mataira, wengine wafe, na Jehanum uende.
Kwa hiyo kwa Yesu unakuwaTajiri na ukifa mbinguni unaenda. “Hakika ni Raha.”
2. Ni Utajiri Udumuo, na Wenye Heshima, ( Mithali 8: 18 Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. )
Heshima maana yake ni kwamba Mungu au Mbingu zitakuheshimu kwani utajiri wao ni sehemu ya utumishi, popote penye Yesu, pana jina lake, na Mungu husema kwamba huwaheshimu wanao muheshimu, pia huwaheshimisha wanaomtumikia.
Licha ya hivyo pia utajizolea heshima tele kwani utajiri wakipepo huweza kukufanya kudharaulika, sasa kama una fedha lakini una mashariti ya kuvaa ndala, au una lala chini, au unapewa mashariti ya kutokumpa mama au baba au ndugu yako fedha yoyote ile, hapo utajizolea heshima au lawama ?
Mstari unafuatia bada ya huo unataja jambo kubwa sana katika dhima hii ya utajiri utokanao na nguvu za Mungu:
Mithali 8: 19 Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu hupita fedha iliyo teule.
Tunaambiwa kuwa Matunda ya Mungu, au ya huo Utajiri utokanao na Nguvu za Mungu, unapita Dhahabu tena ile safi, Matunda maana yake ni mafanikio, Pia Faida yake hupita fedha teule, Biblia ya Kingereza haijatumia neno fedha kwa maana ya Shekeli au pesa, bali andiko hilo humaanisha madini  aina ya fedha,
KJV: “.. and my revenue than choice silver.
Kwa mantiki hiyo ni kwamba utajiri unaotoka kwa Mungu unadhamani kubwa sana kuliko madini yanayopatikana katika dunia hii, wanariadha au wanaoshiriki mashindano kadhaa ya ulimwenguni wanafahamu wanaoshika nafasi ya kwanza hupewa Medali ya Dhahabu, na wanao fuati hadi namba 3, ipo ya Shaba na Fedha, kwa hiyo Utajiri huu umebeba heshima kubwa katika uso wa dunia hii, sema watu wengi hawajaijua hii siri, na wanaoijua wanaikwepa maana wanasema kwamba utajiri wa Mungu unakawia, ila wa Shetani ni wa papo kwa hapo.
“Easy Come, Easy Go.” Licha ya hivyo pia utajiri wa Shetani kuutegemea ni hatari sana, kuna watu wamejiunga na hizo dini za mashetani ili wapate mvuto wa kisanii, kibiashara na hata kiuongozi lakini wameishilia kubaya, wapo waliochukuliwa au kuibiwa nyota zao huko, wengine, kutumikishwa tu.
Kuna Mchungaji mmoja hapa nchini Tanzania anaitwa Mchungaji Joji, huyu anakiri kuwa alikuwa ni mwanachama wa “Freemson” ambayo ni dini ya mashetani, anasema kuwa aliingia huko ili kujipatia Utajiri, lakini hakupewa bali liishilia kupewa kazi ya kuwalinda watu waliochukuliwa mteka kishirikina ili wasitoroke.
Amesota huko miaka ya kutosha, lakini hakuambulia kitu bali ni utumwa tu. Kwa hiyo kwa Shetani kuna kupa au kukosa.
Sasa ni kweli Mungu unaweza kuomba fedha leo asikupe leo, bali akakupa hata miaka kadhaa ijayo, lakini sababu yake kubwa, ni hii:
1. Mungu hataki ungamiye, Fedha ukiipata kama huna maarifa ya kutosha inaweza kukupoteza au kukuangamiza, Kwa hiyo anachokifanya cha kwanza ni kukupatia maarifa, aidha kwa njia ya mapito au mafundisho, kwa wana wa Israeli anatuambia kwenye kumbukumbu la Torati kwamba aliwaacha miaka ile  40 jangwani woane njaa, ili wafahamu kuwa mtu hata ishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana.
Kumbukumbu la Torati 8: 3 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana.
Hekima hii inalenga kumsaidi mtu kwamba hatakiwi kuweka tumaini lake kwenye mali au fedha ama vitu, kwani sivyo vinavyotupa kuishi bali ni Imani ndiyo itupayo kuishi.
Ayubu alilifahamu hili jambo sana na kuliishi, maana alipopita kwenye nyakati ngumu hakukata tamaa, bali alisema Bwana ametoa na yeye ametwaa, tena jina lake lihimidiwe, pia kuna mahali anatuambia kuwa hakuweka tumaini lake kwa dhahabu au mali zake;
Ayubu 31: 24 Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu;
25 Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi;
26 Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea katika kung'aa;
27 Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu;
28 Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu
.
Maandiko hayo yanatupa dhima kubwa sana kwamba Ayubu aliijua hii siri, ndiposa Mungu akamuinua.
Kwa mantiki hiyo Mungu anafahamu fika ni lazima ampitishe kwenye shule maalumu tu ayetaka kumuinua, Yakobo alikaa kwa Labani miaka 20, ili ajifunze, Wana wa Israeli walisota jangwani miaka 40, andiko tulilolisoma hapo na ukisoma hiyo sura kiumakini ya Torati utajionena kwa Mungu alinuia kuwafunza jambo kubwa sana.
Kufanikiwa kwa mtu ambae hana Ufahamu au Maarifa ni kuiangamiza nafsi yake, au maisha yake, au hali yake ya kiroho;
Mithali 1: 32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
Ukitaka kuamini kuwa jambo hili ni kweli, tazama kuna watu wanafanikiwa kanisani hawaendi tena, kuna watu wanafanikiwa hawaimbi tena kwaya, kabla ya kuwa na kazi alikuwa akihudumu, alikuwa akija kanisani kila siku, alikuwa akitembelea wengine, ila toka amejenga nyumba tena vyumba viwili, kanisani haji tena, akiulizwa anajibu kuwa yupo “bize”.
Huko ndiko huitwa kufanikiwa kwa mpumbavu, kuna wanaume ambao kabla ya kazi walikuwa wakiwahi nyumbani, ila toka biashara zimechanganya hawakumbuki tena kurudi nyumbani hata huamua kulala nje, na mke akimuliza anakuwa mkali kweli kweli.
Kuna wake kabla ya kufungua bishara au kupata ajira walikuwa wapole, walitii na kuwaheshimu waume zao, ila baada ya mambo kukaa sawa kiuchumi, kiburi kimeinuka kama kile cha Lusifa baba yao, naye anadai haki sawa ndani ya nyumba, toka anunuwe kibajaji basi kila siku ndani hakuna amani, ana mdharau mume hata kumuita, “mwanume gani wewe, mwanaume suruali, mwanaume maono matupu, una ndoto nyingi lakini hata 10 mfukoni huna”, na kabla ya kuinuliwa alikuwa akimtii na kumuheshimu, ila sasa amekuwa ni bingwa wa kiburi.
Sasa huko ndiko hitwa kufanikiwa kwa mpumbavu, ni sawa na mtu aliyeyaona matunda na kuvua viatu kisha kukwea mtini, muda wa kuondoka akaondoka na kuacha ama kusahau viatu hapo chini ya mti, huyu hata fika mbali maana jua na miiba itamdhuru njiania.
Sasa ili usikumbwe na adha kama hiyo Mungu huamua kukupitisha darasani, ila Shetani hana haja na kufanya hivyo maana anajua hata kama ulikuwa mpole, na mchaji, akikupa tu mali hata yeye akikaa mbali, kwa kuwa ni mpumbavu, itakuangamiza, ndio maana kwa wale wenye maarifa walau kiduchu, huwazungusha sana katika kuwatajirisha, hadi afunge nao maagano makuwa ama makali ambayo anajua hawataweza kuchomka kirahisi.
Fahamu kuwa mali ni roho, ndiposa Mithali husema kuwa inajifanyia mbawa na kuruka huku na kule, hakuna kitu kisichokuwa na mwili kiwezacho kuruka;
Mithai 23: 5 Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.
Pia ushahidi mwingine kuwa mali ni roho, ni kwamba maandiko husema kuna watu wanaangamia kwa udanganyifu wa mali, ikiwa na maana kuwa mali hudanganya, hakuna kitu kisicho na uhai kiwezacho kusema uonga, maana ni shariti kiwe na kinywa, ndiposa kitowe maneno, na maneno ya uongo yana hila ndani yake, kwa hiyo fahamu na akili lazima zihusike katika kupangilia au kujenga hizo hoja za hila;
Mathayo 13: 22 Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Ndio maana mtu ambaye amedanganywa na mali, ukimuliza mbona jana hukuja ibadani, hata kosa sababu ya hila au ya uongo ya kukutupia, utamsikia akisema kuwa kazini tumebanwa, wakati anajua kwamba angeomba ruhusa au muda wakuja ibadani angeweza kuupata, lakini pia mwingine atajitetea kuwa alienda kupokea mzigo angali angeweza kumtuma mtu ama kutumia muda mwingine kufanya hivyo, ama wana kikundi chake cha fedha au wenzie walikuwa wakikutana siku hiyo, sababu huwa nyingi, na ukitaka kujua kuwa zina hila ndani yake, akiulizwa na huyu hujibu vile, na akiulizwa na mwingie katika nyakati au siku tofauti huwa na jibu jingine, au kila uchwao haishiwi sababu.
Ukiona hayo fahamu kuwa mali imemdanganya.
Lakini pia wasomi wa Biblia wanafahamu kwamba maandiko husema kwamba hazina yako ilipo ndipo na moyo wako ulipo, mana yake ni kwamba mali huweza kukaa mahali kwenye ulimwengu wa roho, kisha kuufanya na moyo wako kukaa hapo;
Mathayo 6:21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Kwa mantiki hiyo ni kwamba Mungu lazima akupitishe kwenye hii suhule ili kukutengenezea mazingira ya kuiweka fedha yako kwa Mungu, usipotoa sadaka, usipomuheshimu au kumuabudu Mungu, maana yake unaiondoa hazina yako mbele zake, kwa mantiki hiyo na moyo wako utaondoka mbele za uso wake, nimelishuhudia hili sana, kwamba kuna watu kabla ya mali walikuwa wachaji wa zuri sana, ila bada ya kuinuliwa, wamemsahau Mungu, na sababu kubwa hapo ni mali yao waliiondoa madhabahuni, nayo kuwandoa kwa Mungu.
Sasa Mungu hataki kukupoteza ndiposa hana haraka katika kukutajirisha, maana kwake kilicho cha msingi ni wewe kumtumikia kisha kuuridhi ufalme wa mbinuni, kiblia utajiri ni ziada, ukitaka kuamini kamulize Petro alipomwambia kuwa tumeacha vyote na kukufuata wewe je tutapata nini?
Kuna jibu alipewa pale, lakini kanuni ya kwanza kumbe ilikuwa ni Peto kuacha vyote, kisha kuzidishiwa kuje, wengi hutaka kuzidishiw kwanza, kiblia haku Kanani bila Jangwa, ukilikata Jangwa na Kanani pia umeikataa, hali hii ya kukosa ustaimilivu wa jangwa ndiyo huwafanya wengi kumkimbilia Shetani, ili hawafahamu kuwa uangamivu na mauti imo humo.
(Mithali 7: 27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.)
2. Mungu anataka kuikuza akili yako, Wagalatia 4: 4.1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;
4.2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.
Mtoto mdogo ukimpatia fedha atakimbilia kununua pipi, au midoli, alikadhalika kwa waliokoka kama bado hawajafikia kiwango cha kufahamu kusudi la Mungu kuwa tajirisha huwa kama watoto, ndiposa wengine huwa wazito kutoa fungu la kumi, huu ni utoto, maana hawajui kusudi la kutajirishwa na Mungu wao, Wengine huwa na tabia za kujivuna mara baada ya kuipata fedha, hudharau wengine na hawakumbuki kuwasaidi wahitaji, wakati ama kipindi kabla hawaja fanikiwa walitoa ahadi ya kufanya hivyo, nakuguswa kukufahamisha japo kwa kifupi maandiko yanayoelezea kusudi hili:
1 Timotheo 6: 6.17 Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha.
6.18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;
6.19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Sababu zipo nyingi ila hizo ni miongoni mwazo, sasa kukusaidia ili muda wakupitishwa au kufundishwa na Mungu usiwe mkubwa, unapaswa kuhakikisha unakuwa muombaji, pili msomaji wa Neno la Mungu, tatu hakikisha unafuatilia masomo ya maarifa kiuchumi, na kusoma vitabu vya mafanikio kiroho kiuchumi ikiwemo kile cha kwangu cha TAJIRIKA KIBLIA.
Na muombe Mungu akupe kupita vyema kwenye hilo darasa, kisha hakikisha unakuwa mvumilivu na asiye muoga au mnung’unikaji, wana wa Israeli Mungu alikusudia kuwapitisha jangwanikwa muda mfupi sana, ila walinung,unika, na kuishiwa na uvumilivu pamoja na kuyaogopa yale majitu, Mungu aliwaongezea muda, nawe epuka mambo kama hayo ili kupita kwa muda mfupi.
Kumbuka msingi mkubwa wa andiko la pwenti yetu kuu hapa unatokana na lile andiko la Utajiri wa Mungu una Heshima na niwakudumu la Mitali 8:18, tumelitazama sana jambo la Heshima sasa nataka kukufafanulia lile la kudumu:
Utajiri wa kiungu ni wakudumu kwa sababu hauchuji, wala mali yake haipuputiki, ama kuangamia kama ile ya kipepo, ambayo mwenyewe, akifa hufa nayo.
Ukisoma maandiko utajionea kwa mapata sana jinsi ambavyo watu waliofanikiwa kibiblia walivyowarithisha watoto wao utajiri, licha ya Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kisha wakina Yuda, Yusufu, Manase, Efrahimu na kadhalika, pia yupo Mfalme Daudi, ambaye alimrithisha mwanae Sulemani Ufalme na mali kedekede;
1 Mambo ya Nyakati 28: 11 Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na orofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;
12 na mfano wa yote aliyokuwa nayo kwa roho, katika habari ya nyua za nyumba ya Bwana, na ya vyumba vyote vilivyoizunguka, ya hazina za nyumba ya Mungu, na ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu
.
Ukiendelea kusoma utajionea jambo hili kimapana zaidi, hapa tuna pata dhima nyingine ya kuridhishwa hadi utumishi, nje ya ile ya Utajiri.
Lakini nawiwa kukusisitizia kuwa Utajiri na Heshima hutoka kwa Mungu, andiko lile la Mithali liliandikwa na Mfalme Sulemani, nakupa andiko ambalo la baba yake yaani Mfamle Daudi alilonena vivyo hivyo tena aliongeza na vitu vingine kama nguvu, na uweza, ambavyo ndivyo vilivyobeba kitabu hiki, nikiwa na mantiki kwamba kwa Mungu kuna Uweza na Nguvu inayotuwezesha kutawala na kumili kwenye ulimwengu wa roho, kwa hiyo hakuna haja ya kutegemea nguvu za miungu mingine angali ipo nguvu iliyo salama;
1 Mambo ya Nyakati 29: 12 Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.
Kumbe ! Kwa Yesu tunatukuzwa na kuwezeshwa! lakini sio kila mtu, bali ni yule aliyeamua kumtegemea Mungu. Nasio kidini, Hapana! Bali ni katika Roho na Kweli, Yaani kuokoka na kumaanisha, haswaa.


Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPAhttps://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)
Tafadhali kitabu kikitoka usikikose


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni