Leo ninakuletea tu Utangulizi wake, na niyangu rai kukutaka kufuatilia kitabu hiki punde kikiingia Sokoni, pia kwa dhati kabisa ninaomba maombi yako ili nikikamilishe vyema na tena kwa wakati.
Utangulizi:
Kukataliwa maana yake ni kukosa kibali. Hali inayokufanya kukosa mvuto mbele ya wahusika, kutokudhaminika, au kuwa na dhamani ama sifa ama kupata heshima stahiki kutoka kwa jamii inayokukataa ama kukubagua.
Kuna vitu watavifanya bila kukushirikisha angali ulistaili kufanyiwa hivyo, ukisoma kisa kile cha kupakwa mafuta kwa Daudi, utaona kuwa watoto wengine wote waliitwa ila Daudi pekee hakuitwa kwani alisaulika;
1 Samweli 16: 10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Tatizo la kukataliwa huwalinaumiza, linajeruhi, na kumuacha muhisika akiwa katika hali ya unyoge, na kukosa raha, na hali hiyo hiyo ya maumivu ispopata tiba ya haraka huweza kusababisha madhara makubwa mno katika kiroho cha mtu na kimaisha kwa ujumla.
Daudi ni miongoni mwa watumishi walikumbwa na hali au na kadhia hii kwenye Biblia, pia imo kwa Musa, Musa alitaka kuwakomboa wana wa Israeli maana mmoja wao alipoonewa na Mmisiri alihakikisha anamuwa yule muonevu, na alipowaona wao kwa wao wanapigana alijaribu kuwapatanisha, lakini yule muonevu alimgeukia na kuibua hali ya kumkataa Musa kama muamuzi, jambo lililochangia kutoroka au kuikimbia ile nchi, ingawaje sababu nyingine ni hofu kwa Farao, ila na hii ilichangia, maana hakuwa na makazi tena yaliyosalama, kwa Wamisiri Farao anawinda roho yake, na kwa Waebrania wenzake, hawamtaki.
Wapo watu hivi leo wanaokataa kwenda kwao kabisa, au kushirikiana na ndugu zao, na wengine kuhama kabisa makanisa kwa sababu ya kukataliwa, na anajiona hana dhamani kwao, ama hana kibali kwa Mchungaji au watumsihi fulani kwa hiyo hana budi kuhama hapo, na kwa bahati mbaya hata huko anakohamia roho hii inamfuatilia, Ashukuruwe Mungu haikuwa hivyo kwa Musa, maana Midiani alipata kibali, Daudi kwa Wafilisti alipata kibali, na hatimae kupanga mipango ya kuitwa Israeli.
Lakini wapo wapendwa ambao kila wanapoenda, hawakubaliki, hali ya kukataliwa imekuwa kama mkosi au mzimu unaowafuatilia kila waendako, wakipanga nyumba pale lazimakutokee jambo, wakihamia mtaa fulani, chokochoko haziishi, ukiona hivyo jua ipo roho inayokufuatilia nyuma, na huna budi kuishinda.
Lakini kuna aina mbili za kukataliwa, pia zipo tatu, (a) Kama Roho Kutoka kwa Shetani, ambayo ndiyo iliyonisukuma kukuandikia hiki kitabu, pia (b) Adhabu ya Mungu, Mungu alimuadhibu Kaini, na Kaini aliomba apunguziwe adhabu, Mungu hakuiondoa ile hali au roho ya kukataliwa juu yake, bali alimuweka alama, maana yake ni kwamba atakayemdhuru Kaini naye atakuwa ni sehemu ya ile hali au ya laana ya Kaini.
“Kwa bahati mbaya hata leo wapo watu wanaojichotea hii roho au laana aidha kwa kutenda dhambi ya Kaini au kushirikia tukio la kumcheka au kumpiga Kaini.”
(c) Kama Hali, Uduni wa mtu, Ufukara, au jinsi anavyojiweka, Ulemavu ama Ugonjwa, fulani huweza kumfanya mtu huyo kukumbwa na hali fulani ya kukataliwa.
Katika (a) iliyoba aina kutoka kwa Shetani, nataka kukufahamisha kuwa nayo imegawanyika katika pande kuu mbili;
(i) Juu ya Mtu, Jambo hili au hali hii humkuta mtu, na huweza kuwa ndani yake kabla hajazaliwa, anapozaliwa, katika maisha yake yote, kama shuleni, na wengine hujikuta wakikataliwa na marafiki, wapendwa, au wengine huwa ni kwa ndugu tu, na wengine ni katika kazi, au shuhuli fulani za kiuchumi, nikipata kibali nitakujuza ni kwa nini Shetani hulenga sana sehemu fulani.
Mfano wapo ambao ni kwenye ndoa tu, kiuchimi, kihuduma hana shida, ila ndoa ni mwiba, mke au mume, amegeuka adui, na baba mkwe na mama mkwe, ama ndugu fulani wamume ama mke.
Pia wegine kwenye ndoa ni Shwari, ila kwenye Huduma yaani wapendwa wenzake, watumshi wenzake, ama Mchugaji wake, ni kama Paka na Panya, ingawaje wanamkubali yupo vizuri kiroho na kihuduma.
Mwingine ni kwenye Elimu, hapo napo pamegawanyika, wengine ni kwa walimu tu, wengine ni kwa wanafunzi, na wengine shida ipo kwa wazazi, wanazo fedha lakini hawataki kumlipia ada, au kumpa mahitaji ya kielimu, na kwa bahati mbaya wapo ambao imechanganyika, wanafunzi wenzake hawampendia, na walimu wamemsusa, huku wazazi wakimpiga vita, wanataka asome, lakini hawampi ushirikiano sahihi.
Nisikilize: Mimi ninafahamu mambo haya kiundani sana, maana ni hali ambayo nimekuwa nayo;
Shetani anapoleta vita kwenye Elimua, kwa kuachilia roho yake ya kukataliwa, jua Hatima ya maisha yako yanahitaji elimu, ili kufanikiwa.
Mimi nimefukuzwa shule mara mbili nikiwa nasoma darasa la tatu, baadae kuhamishiwa shule nyingine na kuanza dara sala pili baada ya kukaa mtaani mwaka mmoja na kuanza maisha ya kichokoraa, napo hapo nilifukuzwa nikiwa dara sa pili, kwa mwalimu kusema nipigwe mawe kama mwizi, tena bila kosa lolote lile.
Nimesoma shule tatu za Msingi, ile ya Ilala Boma pale Dar es Salaam, na Kifufuu na Maharo zote za Rombo Mkuu.
Nikiwa darasa la 5, mwalimu aliniambia kuwa nikifika mwezi wa 12 ningali shuleni nikachinje mbuzi, ikiwa na maana nikatowe kafara, maana wachaga wakifanikiwa katika jambo fulani hutoa kafara, kama sisi tunavyotoa sadaka za shukurani mbele za Mungu wetu.
Hakuna aliyeamini kuwa ningemaliza shule ya msingi; Nikiwa dara sala 6, mama yangu alishiriki kosa bila kudhamiria la kunipiga viboko vingi huku akitaka apewe karatasi ili aweke sahihi ya mimi kuacha shule, ila nilisema ninayo ndoto maishani mwangu, kwa hiyo sitaacha shule, baadae aliniomba msahama maana kuja kwake shuleni ni wito wa mimi kupigwa na mwenzangu nakutoka damu za puania, wala sikurusha ngumi wala kulipiza kisasi, sasa wakati ninahojiana naye nyumbani nilimuliza kosa la mimi kuchapwa ni lipi wakati mimi ndiye niliyepigwa, na mtuhumiwa wakunipiga hakuhojiwa wala kilichomfanya kuitwa shuleni hakukifanyia kazi.
Nikiwa mdogo mtu mmoja mwenye dhamana ya kutulipia ada alitamka maneno haya, kuwa mdogo wangu asipofaulu atampeleka shule binafsi, ila mimi nisipofaulu nitapelekwa ufundi, nilipinga jambo lile sana, na nilitamka kufaulu.
Ilikuwa kila nikikiri kufauli darasa la saba watu wanacheka, maana waliniona mimi niwa ufundi tu, ingawaje kweli nilipokuwa darasa la 4, na la 5 nilikuwa nikiweza kujenga nyumba na hata kupiga sadakafu na “plasata” kuta, hata “sling-bodi” fulani pale nyumbani mimi niliiweka na sakafu.
Niliumia sana, moyoni nilikuwa na ndoto kubwa, ambazo nilijua zinahitaji elimu, sio ya ufundi bali kama hii niliyo nayo leo, lakini Shetani amechilia roho ya kukataliwa inayokuja na mtazamo mwingine juu yangu, kuwa mimi ni wa ufundi tu, ila mwenzagu ni wa Sekondari kisha Chuo.
Nikiwa kidato cha kwanza mwalimu mmoja akasema kuwa wenzangu wanishauri na kuniombea sana maana sitaingia kidato cha pili bila kufukuzwa, ilikuwa kila siku ya haliamisi lazima niingie katika adhabu fulani, na kila jumanne Mungu alikuwa akinijulisha lijalo, kuna wenzangu nilikuwa nikiwafahamisha kuhusu swala hilo nao walikuwa wakiniona kama mwenye nguvu fulani za kiroho maana niliweza kujua yajayo.
Mama yangu mzazi hajasahau hadi leo alipokuja katika nyumba nilipopanga nikiwa nasoma natumai kidato cha pili mwishoni au cha tatu mwanzoni, alinikuta katika hali ya kutisha, yenye dhiki kubwa sana, na ni baada ya walimu kumtaka kuja, hali iliyompa mzigo na masukumo mkubwa wakuniombe sana.
Nilianza maisha ya sekondari kwa kulala chini, koti langu fulani kubwa ndilo lililokuwa kitanda, godoro, na shuka, na “blanketi” langu, Sikuwa na kitanda wala godoro, na mnafahamu maeneo ya Kilimanjaro yalivyo na baridi tena mbaya zaidi ukilala chini.
Niliishi maisha magumu sana, ikiwemo ya kusimamishwa shule bila hatia, na kuingia katika vizingiti vya Ibilisi.
Safari yangu haikuishia hapo tu, bali hata nipokuwa chuo, nilikuwa ni mwenye vita kubwa sana, hususani kutoka kwa walimu, katika yote hayo Mungu alinishindia, na kulikuwa na walimu walikuwa wakija na kunifahamisha kuwa jamaa au siku fulani mwalimu fulani na fulani walikaa kikao ili ufukuzwe shule, lakini Mungu alinipigania.
Muda huu roho Mtakatifu ananikumbusha tukio moja ambalo ni gumu lakini nililivuka kwa imani kubwa sana.
Siku moja, nilitwa ilinipewe barua fulani, sikuijua haswa ni ya nini, ila nilisimama nje kwenye ofisi ya “Secretary” wa chuo nikiwa nje ya ile ofisi macho yangu yalichungulia kwenye “Komputa” na kumuona akiandika barua yenye hiki kichwa;
YAH/ KUMFUKUZA OSCAR SAMBA CHUO. Haikuwa jambo jepesi, ila sikujua mahali ujasiri ulipochomokea, niliomba kimoyo moyo na kupinga jambo lile huku nikimuomba Mungu mimi ninakataa kufumkuzwa chuo, maana ninayo maono nayo yanahitaji elimu.
Mara gafla mwalimu husika akaingia kwenye ile ofisi na kuteta maswala fulani, na kabla ya hapo nilimuoa muhusika aliyekuwa akiindia akitoka na kuingia kama mtu mwenye roho ya mahangaiko ama kuku anayetaka kutaga na mahali pake kutwaliwa ama mama mwenye uchungu wa kuzaa, kisha baada ya Mwalimu huyo kuingia nilipochungulia tena niliona ikiwa na kichwa cha kunitaka nikamuite mzazi.
Nilingia kwenye maombi baada ya barua hiyo, nami nilimuita Binamu yangu Foltunatusi ili asimame nafasi ya mzazi, cha ajabu katika kikao kile, hakukuwa na la heri wala la shari, bali mkuu wa chuo alisema kuwa kijana huyu hana tatizo, na ni mtu muhimu sana kwetu sisi na kwa taifa, maana ndani yake kuna uongozi, na tuna mtarajia kuja kuwa waziri au mbunge, kwa hiyo hapa hakuna kosa lake, wala hakuna wakuhukumiwa.
Kuna watu wamefukuzwa shule sio kwa sababu walikuwa wakosaji la! Bali ni kwa sababu Shetani aliachilia roho ya kukataliwa juu yao, na roho hii ikiwa juu yako hata kama huna hatia watakuhukumu kwa hisoria, watasema haiwezekani kila kosa ni wewe tu. Katika roho hii kuna aina nyingine ya kukataliwa nayo ni hii;
(ii) Kama Sehemu ya Upinzani katika huduma, Jambo hili halikwepeki, kila aliyeitwa na kila aliyeokoka ni lazima akutane nalo, kwa kifupi hivi ni vita katika Utumsihi wa Mungu.
Hii ndiyo roho iliyomua Yesu, na ilimfanya kufuzwa katika maeneo kadhaa, Ukisoma kisa kile cha kuponywa kwa Mgelasi, yule aliyekuwa na jeshi la mapepo, utaona kuwa watu wa ule mji walimtaka Yesu aondoke mipakani mwao, kisha Yesu aliondoka.
Kuna mahali Yesu aliwataka wanafunzi wake kuwa katika miji watayoiendea ili kuhubiri injili wakiwakataa wakung’ute mavumbi yao huko, hayo ni miongoni mwa madhara ya kumkataa mtumishi au kushiriki hii dhambi;
Mathayo 10:13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
10.14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.
10.15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.
Luka 10:16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
Lakini pia anatuambia kuwa hawatukatai sisi, au hakukatai wewe bali wanamkataa Yesu, kwa mantiki kwamba hutakiwi kutishwa na kukataliwa Mopendwa, haijalishi ni ndugu, kama ndivyo hata Yesu ndugu zake waliwahi kumkataa, wakisema kuwa amerukwa na akili, pia haijalishi ni watu wa nyumbani kwako au kijiji kwenu, Yesu alipohubiri Ijinili kule Kaprinaumu walimkaa na Yesu kusema kuwa Nabii hakubaliki au hakosi kuwa na heshima isipokuwa nyumbani kwake, nawe usijali, maana kuna majira watasema kuwa huyu ni mwana wa Mungu. Yaani watakiri kuwa ni kweli Mungu amekuita.
Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry #SHARE #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Kama hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na BWANA kwa upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU, ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com
Pia #Like #Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
PAGE: https://www.facebook.com/ugukombozigospel/
Kikundi: https://www.facebook.com/groups/2268418230050621/
Pia kwenye mtando Mpya wakitanzania wa
2 DAY SKY: https://www.2daysky.com/ukombozigospel
Pia TAZAMA VIDEO ZETU HAPA https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)
Au www.mwalimuoscarvitabu.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni