Na Mwalimu Oscar Samba #UgMinistry #SHARE #SAMBAZA Ili kueneza injili hii Zaidi.
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO NAYO.
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO NAYO.
Kama
uliwai kuua mtu, kwa kukusudia au bila kudhamiria, kwa njia ya ajli, au kutumia
silaha, kutoa mimba, ukiwa kama mama wa mtoto, baba, dakitari, au kushiriki kiushauri
ama kiuwezeshaji ama kwa njia yoyote ile.
Pia hata
kama ulihusika katika mauaji ya mtu au watu, kwa njia yoyote, ikiwemo ya
ushauri, kupanga mipango, au unafahamu fika na bayana kuwa damu ya mtu fulani
ipo juu yenu, au juu yako, au katika eneo unaloishi njia hii itafanyika msaada
kwako au kwenu Lakini pia hata kama wewe ni asikari, au mwanajeshi, na uliwai
kumwaga damu, haijalisha uliona ina hatia au la, ila ujue ukweli wa hatia hiyo
na uhalali wa mauaji hayo anayefahamu ni Mungu mwenyewe, Shetani na damu husika
, kwa hiyo nawe yafanye haya maombi, ukijaribu kujihesabia haki kuwa ulikuwa ukitimiza
wajibu wako sawa, au uliwajibika kufanya hivyo na haoni kosa lako, “it’s ok,” ila kwa ushauri wangu na
waimizo la Roho Mtakatifu ndani yangu, huna budi kufanya hivyo:
Hakikisha
unainyamazisha hiyo damu, ili isiendelee kunena mabaya au kulia kisasi au
malipizi kwenye ulimwengu wa roho. Lakini
kanuni ya kwanza;
1. Omba Rehema,
tubia tukio hilo, muombe Mungu akusamehe, wala usijihesesabie haki, kwa namna
yoyote ile. Tumia Damu ya Yesu katika kutubia hilo kosa, ombea rehema kutokana
na umwajikaji wa Damu ya Yesu kwa ajili ya ondole la dhambi, Mathayo 26:28.
Omba hadi upate mani ya kiungu moyoni mwako.
2. Inyamazishe
hiyo damu. Katika maandiko tunaambiwa kuwa damu ya Habili ilinena, ukienda
katika Mwanzo 4: 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Tunaona hapo kuwa hii damu ililia,
ukiendelea mbele yake, unaona Mungu akiachilia adhabu, ikiwa na mantiki kuwa
kilio kile kilihitaji ulipizaji wa kisasi, kwani baada ya kisasi hatuinoni
ikilia tena.
Kwa kuwa
wewe umeshaomba Rehema, ni fika kuwa Mungu amesha kusamehe, au kufuta hilo tukio
kiroho, kwa hiyo unao uhalali wa kutumia Damu ya Yesu ili kunyamazisha hiyo
damu iliyomwagwa.
Tamka
kuinyamazisha kwa kumwaga Damu ya Yesu juu yake na kuitaka inene mema, tumia
andiko la Waebrania 12:24 linalosema kuwa Damu ya Yesu inanena mema kuliko ile
ya Habili.
Omba hivi, kwa jina la Yesu Kristo wa
Nazareth, natumia Damu ya Yesu kuinyamazisha hiyo damu iliyomwagika, “kama
unamjua mtaje jina,” namwaga Damu ya Yesu kwenye hiyo aridhi, kwa Damu ya
Yesu Kristo, ewe damu nyamaza kimya,
milele, ninakuamrisha nyamza kimya, namwaga Damu ya Yesu ile ya Agano jipya,
sawasawa na Luka 20:22, na Matayo 26:28, ninakunyazamazisha ewe damu ya fulani,
pia ninaitaka Damu ya Yesu kunena mema ili kubatilisha sauti za kisasi na maneno
ya malipizi kutoka kwenye hiyo damu ya fulani.
Fanya hayo
maombi kwa imani, huku ukimnyima Shetani kukuhukumu moyoni kuwa uliua, fahamu
toba uliyoifanya tayari Mungu alishakusamehe, kwa hiyo hatia yako haipo tena
mbele za Mungu na Mungu akishasamehe huwa anasahau kabisa. Kwa hiyo hukumu ya
kipepo ipinge kwani inalenga kukuondolea ujasiri mbele za Mungu, na fahamu kwa mujibu
wa Waebrania, tunaambiwa tukisogele kiti cha Neema kwa Ujasiri ili tupate
Rehema, kwa hiyo hakikisha unapingana na Ibilisi katika hili jambo pili nafsi
yako pia isi-kuhukumu, na muombe Mungu ama Roho Mtakatifu aiwezeshe kujisamehe.
3. Futa Madhara
Yote yaliyopenya na yaliyokusudiwa, kunapotokea mauaji au umwajikaji wa
damu isiyo na hatia, kwenye ulimwengu wa roho Shetani hutumia jambo hilo kama
lango la kupenyeza madhara, au matatizo fulani, lakini pia, hata Mungu huachilia
adhabu, ukitaka kuamini vyema, nenda kwa Kaini nawe hapo utajionea haya mambo
vyema.
Kwa hiyo
nyunyiza Damu ya Yesu huku ukitamka kufuta hayo madhara, na kuyachomoa, yaweza
kuwa ni magonjwa, roho ya kukataliwa, mauti kwenye uchumi, mauti kwenye ndoa na
kadhalika.
Chimbuko la
ujumbe huu, ni pale mwanamke mmoja aliyenifuata siku chache zilizopita,
akiniambia kuwa uchumi wa mume wake upo mahali pa gumu, na kubainisha kuwa kazini kwao, kuna mfanya kazi mwenzao,
alisababisha ajali, na aliyegongwa alifariki.
Mara baada
ya ajali hiyo uchumi wa kiwanda umekuwa mahali pa gumu hadi kufikia hatua ya
mishahara ya wafanya kazi kusumbua.
Mimi
nilielewa kwa haraka kuwa damu ya mauti iliyomwagika ilisababisha hayo madhara,
na iliachilia mauti kwenye uchumi wa kiwanda.
Kwa hiyo
ilinibidi kuomba rehema kisha kuinyamazisha ile damu kwa Damu ya Yesu, na
kuitaka Damu ya Yesu inene, mema, nikiwa na maana kuwa ile ya aliyegongwa
ilinena au kulia au kuhitaji mauti kwenye uchumi wa kiwanda sasa hii ya Yesu
itafuta yale maneno, na kunena Baraka, na mafanikio katika kiwanda.
Kama upo makini,
umeshaelewa umuhimu wakutubia hata matukio yaliyofanywa na wengine, kwani yana
matokeo makubwa kwako, kieneo, kihuduma, na hata kikazi kama yapo mafungamano,
pia hata kindugu kama upo uhusiano, kwani mtoto wa Kaini, na mke wake,
wanashiriki matokeo ya adhabu ya baba yao, au mumewe.
Kwa hiyo,
tamka kuondoa hayo madhara kwenye ulimwengu wa roho, hata kama huja yajua, Roho
Mtakatifu atakusaidia kuomba vyema au kukufahamisha pia zuia yaliyokusudiwa yasitokee.
4. Itisha Urejesho, Upatanisho na Matengenezo, Jambo hili liliharibu kasa maisha
ya Kaini, na kwa kiwango fulani maisha ya Mfalme Daudi pale alipomua yule mume
wa mke aliye mtwaa, yaani Uria.
Kwa hiyo,
maadamu Mungu ameshakusamehe, au kumsamehe muhusika, au rehema yake ipo juu
yenu au juu ya eneo husika taasisi na hata kampuni, ni fika unaweza sasa
kumuomba Mungu afanye urejesho kama kuna vitu vilivyo haribika, au kupotea, au
kufa kabisa, kama uchumi, afya kusumbua na hata migogoro, unaweza fanya
urejesho kupitia damu ya Yesu.
Fanya pia
matengenezo, kweye vitu vivyo haribiwa, maana mauti hufanya mauti na uharibifu
mwingi kwenye mengi, kwa Daudi kulitokea mauaji kwa wanae, Amnoni kuuawa na
Absalom, wake au masuri wake, kutezwa na mwanaye, ufalme wake kutaka
kupinduliwa, hata yeye kuvunjiwa heshima, “ingawaje kulikuwa na makosa mawili,
yaani la kulala na mke wa mtu, lakini pia la mauji ya mume wa mtu, lilichangia
mno.”
Pia itisha
upatanisho, kama ulikuwa nami vyema katika kitabu hiki utafahamu kuwa Damu ya
Yesu inafanya upatanisho nami nimekujuza toka hapo awali kuwa kupitia shuhuli
za kikuhani, hapo zamani za Agano la Kale, kuwa ipo dhima ya Upatanisho.
Tatizo hili
la mauaji, lina tabia ya kuleta mafarakano kwenye ulimwengu wa roho, na hata
kujidhiirisha mwilini, kama ni kwenye kampuni, imetokea ajali au mauaji fulani,
au kwenye taifa, kabila na kabila wanapouana, kinachofuata ni watu hao kuwa na
uhasama, au kuchukiana, kitu ambacho ni hatari na kinazuia upatikana wa amani
sana, maana hali hii huenda kizazi hadi kizazi.
Kwa hiyo
jipatanishe na patanisha jamii husika, kupitia Damu ya Yesu, kwa mujibu wa
maandiko tuliyoyaona hapo awali kwenye pwenti zilizotangulia humu kitabuni,
Damu hii ina uwezo mkuwa, na ukizingatia ni Damu ya kuhani mkuu, na kama tunavyo
fahamu kuhani ana dhima ya kufanya upatanisho, wa Agano la Kale walitumia damu
za wanyma na hata za ndege, ila huyu Yesu alijidhamini kwa Damu yale mwenyewe,
kwa mantikii hiyo nguvu yake ni kubwa mno.
5.Futa Alama ya damu ya Mauti na
Adhabu, damu
inapomwagika bila hatia, huwa inaacha alama mahali husika kwenye ulimwengu wa
roho, kwa hiyo ifute kwa Damu ya Yesu, sio katika aridhi tu, bali hata katika
taasisi, kampuni, serikali, na hata, familia au kazi fulani, au mtu binafsi,
kanisa na kadhalika.
Lakini pia,
kuna kuwa na Alama, ya Adhabu, jambo hili utaliona vyema kwa Kaini;
Mwanzo 4: 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa
kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama,
mtu amwonaye asije akampiga.
Unaweza
usilielewe jambo hilo kama utachambua hilo andiko kimwili, maana utaona tu, kuwa
alama hiyo ni matokeo ya maombi ya Kaini ya kwa Mungu au kama kinga ili
asidhuriwe.
Lakini licha
ya jambo hilo ambalo kweli lipo, na lipo dhairi, ila ukweli ni kwamba, umwagaji
damu, huachilia alama fulani ya kiadhabu, ambayo pia hufanyika kama lango la
haribifu.
Ukisoma hapo
katika hilo andiko, utafahamu kuwa hiyo alama inanenewa, kuwa kila atakayemua,
Kaini, atalipizwa mara 7, kwa hiyo alama yake, ilibeba au ilikuwa na mukutadha
wa mauti, uliyotoka na mauti, ambapo tena, una maudhui ya kimauti kwa atakayesababisha
mauti.
6. Funga hilo
Lango la Uharibifu, Fanya maombi ya Malango, kama huyafahamu tafuta kitabu changu
cha MALANGO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
Kwa kifupi,
damu isiyo na hatia ya mauti ni lango la Uharibifu, lilisababisha uharibifu kwa
Kaini, kwa Daudi, kwa Yoabu, na wenzake, (1 Wafalme 2: 5 Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani,
alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri,
na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua,
na kuimwaga damu ya vita wakati wa
amani, akautia damu ya vita mshipi
uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.)
Kwa hiyo
nyunyiza Damu ya Yesu kwenye hilo lango, na tamka kulifunga wakati unanyunyiza,
fanya maombi haya mfumo wa maombi ya vita.
Pia kama ni
mauti au maujia ya kikabla, jamii na jamii, au vuta vya wenyewe kwa wenyewe,
huna budi kuhakikisha unayafanya kwa mzigo zaidi, na ukisha maliza achilia amani
ya Bwana kwenye eneo, jamii, kampuni, mtu au sehemu husika.
Mwisho, Mshukuru Mungu kwa uponyaji wake, na
msamaha, lakini pia nyunyiza, Damu ya YESU, kama ulinzi, juu yako, au katika
eneo ulilokuwa ukiliombea, na ifunge kabisha hiyo roho ya mauti isirejee tena,
au kuendelea kukaa hilo eneo.
Na kama
uliyemuombea, yupo mahabusu, futa kesi kwa Damu ya Yesu, kwani rehema
imesamuondolea hatia rohoni, na kama mmekata rufa, tengua hukumu husika
kimaombi.
Pia kama yupo gerezani yaani amehukumiwa
tayari, na haijalishi amehukumiwa kunyongwa au la! Na hataka kama ni kifungo
cha maisha au miaka mingi gerezani, wewe tamka kufunguliwa kwake, maana hii
Damu ya Yesu, ina huo uwezo, na jambo hili lipo wazi kimaandiko;
Zekaria 9: 11 Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo
lile lisilo na maji.
Cha msingi
ni wewe kuwa na imani ya kutosha, kuhusu matumizi ya hii Damu ya Yesu.
Tumia pia Andiko
la Isaya 61:1, ili kutangaza uhuru wake, au kujitangazia uhuru wako, kama ni
wewe unajiombea;
Isaya 61: 1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta
niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika
moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na
hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Dalili au ishara
zitakazokujulisha kuwa damu iliomwagika ingali juu yako:
Na Suluhu la
kuepukana na mambo haya ni kufuata hatua za kanuni iliyotangulia hapo juu, kama
umeshaifutua, rudia tena kufanya hayo maombi, na ukimaliza, fanya maombi ya
vita dhidi za hizo roho za mauti la lango lake, na lango la ndoto za mauti
ulifunge.
1. Hofu ya Mauti, Ukiona kila ukikaa mwenyewe, au
ikifika usiku, au ukilala, ukitembea, ama ukikumbuka hilo tukio, unaingiwa na
hofu kubwa, fahamu fika roho ya mauti inakufuatilia, na inatumia lango la hiyo
damu.
Ukisoma
katika 1 Wafalme 2, utajione mwenyewe kuwa Yoabu, aliingiwa na hofu kama hii,
na kukimbilia madhabahuni, ila aliuawa hapo hapo.
Ikiwa na
maana hofu inayokuja, inalenga kudai ulipizwaji wa kisasi, kwa hiyo ni vyema
kushuhulikia jambo hilo, maana njia kuu ya mauti ni hofu, na dalili kuu pia ni
mtu kuwa na hofu, woga, ukiona mtu anyeumwa, nakwambia anasikia kufakufa au ana
hofu kubwa sana, jua Mauti imekaribia, kama ni muombaji msaidie.
2. Kuota Ndoto za Mauti, Hali ya kuota upo msibani,
makaburini, eneo lenye maiti, ni dalili ya kwamba lipo lango la mauti linalokufuatilia,
na ndoto hizo huweza kuua, uchumi, ndoa, kazi, na hata kuleta mauti ya kimwili.
Lakini pia
wengine hutokewa katika ndoto na marehemu, na wapo ambao sio katika ndoto bali
wazi wazi, huweza kuwa mchana, au usiku, wapo ambao pia huona kivuli chake,
kumbuka sio yeye, bali ni mizimu, au mapepo ya mauti yanatumia lango la mauti
yake.
Lakini, wengine
hufika mahali pa kupiga kelele, hali ambayo inaweza kuwafanya kuonekana kama
vile wamerukwa na akili au kuchanganyikiwa, mfano utamsikia akisema, “hao, wanakuja
kunichukuwa, hao, hao, nisaidieni, wanakuja,” anaweza kuwataja na majina yao,
au kujikuta kitaja aliowahi kuwaua, wachawi wanateseka sana na kifungo kama
hiki.
Wasio jua
huenda kwa waganga ili kupa msaada, ambapo hatapata suluhu, ila watazituliza,
au kupunga hayo mapepo yaliyokaa kwenye hilo lango la mauti ya damu isiyo na
hati, lakini madhara yako palepale, na udhibitisho ni kwamba baada ya muda hali
hiyo hujirudia tena.
Lakini baya
zaidi mashariti ya mganga huweza kudai agano au kafara ya damu, halia ambayo
italifanya tatozo kupanuka, na kuwa kubwa zaidi kwani umwagaji wa damu nyingi
utaliimarisha tatizo, na kuongeza ukubwa wake, na kuikaza hiyo nira, na kuongeza
idadi ya mapepo.
Ila wanao
jua, wataitumia njia nilizo zitaja humu kitabuni ili kujiepusha na hili tatizo,
wala hawataangaika kutumia sindano za usingizi au kuamini muhusika amerukwa na
akili au kalewa kwa pombe na hata kulogwa ama kutupia majini, bali ni mapepo ya
mauti, katika lango la mauti la damu isiyo na hatia.
Bali wakati
madakitari wanadunga sindano za usingizi, yeye anapabana na tatizo kiroho.
3. Kujiwa na Kumbukumbu za hilo Tukio, kwa wengine wanapo pita eneo
husika, au kila inapofika muda fulani, kumbukumbu hizo humjilia, na wengine
husikia maumivu kama ya moyo kuuma, ila ni katika eneo la kulia la mwili wake,
ukiona hivyo fahamu ni ishara ya roho ya mauti kutumia hilo lango.
4. Uchungu wa Mauti, wapo wanaoua, na wao kujiua, au
kutamani kufa, au kuwa na uchungu iliopitiza au huzuni ya mauti.
Yuda Iskariote
alipomsaliti Yesu alitamka bayana kuwa ameisaliti damu isiyo na hatia, matokeo
yake, ni yeye kumbilia kitanzi;
Mathayo 27:3 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha
kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande
thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.
Kilichofuata
ni yeye kujinyonga, kwa nini? Uchungu wa mauti na huzuni yake;
I Wakorintho 15:56 Uchungu
wa mauti ni dhambi, na nguvu za
dhambi ni torati.
2 Wakorntho 7:10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu
lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia
hufanya mauti.
(Kama wewe
ndie uliyeua, ninakutaka kuomba rehema na sio kujidhuru)
Pia kama
tatizo hili lipo kwenye eneo, au nyumba unayoishi au kufanyia kazi, basi kila
ukiishi hapo, au kufika hapo, utasikia uchungu huu wa mauti, na dawa yake ni
kumwaga Damu ya Yesu kwenye hilo eneo, ukiomba Rehema, kuinyamazisha na kufuta
uhalali wake, na kuitaka ile ye Yesu inene mema.
Kama kuna
mtu aliwi kuua, au kuuawa, na anawatokea mara kwa mara, bila kujali, ni ndugu
yenu alihusika au la, wewe tumia Damu ya Yesu ya Agano Jipya kumwaga juu ya kaburi
lake, au mauti yake, na ukifanya hiyo kwa imani, hatawatokea tena milele,
nimelifanya hili na nimeona matokeao yake, kwa hiyo sikufundishi nadharia bali
ni jambo ambalo ni bayana na hakika.
5. Kuota Ndota ukiwa unakula nae
chakula, au kula na
watu waliokufa, hii ni ishara kwamba, unaishi chini ya agano la mauti, yaani
kuna mtu amekuingiza, au kuliingiza eneo unaloishi chini ya hilo agano au lipo
agano ulilowai kuingia lenye mauti ndani yake, yaani lilosababisha damu ya mtu
asiye na hatia kumwagika.
Kumbuka
unapoenda au mtu anapoenda kwa mganga, na kuhitaji utajiri, kisha kupewa
mashariti ya kumchukuwa mtu msukule au kafara ya damu, ni bayana jambo hilo huwa
ni agano la mauti au la damu.
Sasa kama
umeajiriwa, au kufanya kazi kwenye kampuni kama hiyo, ninakutaka kujitenga na
hilo agano, kwa maombi ya Damu ya Yesu, lakini kama umerithishwa au kuinunua
hiyo kampuni, ni fika hilo agano unapaswa kulifuta, kwa maombi ya rehema, na
yakulifuta kwa Damu ya Yesu, tubia ufanyikaji wake kiundani katika kuomba rehema,
na yafanye hayo maombi kwa kuugua.
Kumbuka kama
unafanya kazi kwenye hiyo kampuni, au biashara au ni muajiriwa hapo, na
kufahamu lipo agano la damu, sija kwambia, ulivunje, ni elewe, wala usijifanye
wa kiroho kuko mimi au Roho Mtakatifu, nimekwambia jitenge, ila kama kampuni umeinunua
wewe, au kuirithi, hapo unapaswa kulivunja.
Na ukimuona
mtu kama huyu, kama ni muajiriwa, mtenge na hili agano kimaombi, kama ni nyumba
uliyo panga kitenge chumba chako au eneo unaloishi kwa Damu ya Yesu.
Udhibitisho
wa kuwa ndoto kama hizo, za kuota unakula chakula ni ishara ya uwepo wa agano
la mauti, upo katika kitabu kile cha Mathayo 26, na Luka 22, katika karamu ya
Yesu, Yesu alimega mkate, kumpa kila mwanfunzi wake na mzao wa mzabibu, akisema
jambo hilo ni ushirika wa kiagabo, na yale maji ya mzabibu, katika Luka 22:20,
na Matahyo 26:28 tunaambiwa ni Agano jipya, lakini ukitazamwilini ni chakula na
shurubati au “juice” kwa kingereza.
Lakini pia yawezekana
ni agano lilofungwa na babu zako, au baba zako, au jamii ya kwenu, cha muhimu
ni wakina nani unaowaota, na mahali gani au moyoni mwako unashudiwa kuwa ni wakina
nani.
Usijaribu
kupuzi mambo haya, maana yasiposababisha mauti ya kimwili, huweza kuwa ile ya
kiuchumi, na hata kiroho, au kiafya ama kihuduma.
Kuna watu
wakisha ota hivyo, gafla hali ya kuhudumu au utayari wa kufanya huduma
unapotea, au kufifia na hata kufa, au anapoteza ile ladha ya kusoma biblia, kufanya
maombi au utumishi fulani, na Roho Mtakatifu ananiambia hata ushirika na wapendwa
wenzake huadhirika pia, akiwaona atwakwepa, atakwua mziato kuchangamana nao, na
huweza hata kuondoka nyumbani akijua atakuja, cha ajabu hana hata sababu ya
msingi uzito tu unakuja moyoni na nafsi mwake na ni hatari zaidi ukiingia hadi
rohoni.
Ukisoma
vyema hayo maandiko ya karamu ya Yesu utabaini kwamba, jambo lile lililenga kuwa
na ushirika pamoja na Kristo, ndio maana hata leoa, tunatakiwa kufanya hivyo,
yaani kushiriki meza ya Bwana.
Licha ya
hivyo, katika Yohana 6. Tunataarifiwa, ili tuweze kuurithi uzima wa mielele, ni
lazima tuule mwili,wake , na kunywa Damu yake.
Kama kwa
Yesu lililenga kutupa ushirika pamoja naye, ni bayana hata kwa Shetani linanuia
kumfanya huyu mtu kuwa na ushirika na mizimu, au roho za kuua huduma, kiroho
ukisha ingizwa kwenye ushirika na nguvu za giza ni dhairi kuwa hali yako ya
ushirika na Kristo Yesu, itafifia.
Ndio maana
kulitoa pepo lililoingia ndani ya mtu kwa njia ya chakula, au akiota ndoto anakula
au kunywa na watu, huwa linasumbua sana, na ukitaka hauweni ya haraka,
mnyeweshe huyo mtu Damu ya Yesu ile ya Agano Jipya.
(Lakini pia
fahamu sio kila ndoto ya kuota unakula, ni ya kipepo, nyingine huwa na ujumbe
wa Mungu, zaidi tafuta kitabu changu cha NGUVU YA NDOTO KWENYE ULIMWENGU WA
ROHO.)
NB: Ukigundua eneo au aridhi uliyonunua, kuwa ina Damu
ya Mauti juu yake, yaani iliyomwagika bila hatia, ama kitu ulichonunua, au
biashara uliyo nayo, gari ulilorithi na hata nyumba, huna budi kuhakikisha
kuwa, utafuata hizo kanuni za kujinasua na hilo dhara, kwani hata kwa kiwanja au
eneo lilonunulia kwa fedha za usaliti wa Yesu alizopewa Yuda, lilitwa konde la damu;
Matendo ya Mitume 1:18 Basi mtu huyu
alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake
yote yakatoka.
1.19 Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile
likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.
Unaonaje
kama wewe ukija kununu kiwanja cha konde la damu na kuishi hapo bila kushulikia
hilo tatizo?
Utashanga roho
za mauti haziachi kubisha hodi kwenu, nyumba nyingi zenye matatizo, ambazo hazikaliki
au zenye mauza-uza, au majini, zina hili tatizo.
Kama
hujaokoka na unataka kuokoka ama ulirudi nyuma kiroho na unataka kutengeneza na
BWANA kwa upya leo, tafadhali fuatisha nami maneno haya kwa Imani, Sema: BWANA
YESU, NINAKUPENDA, NINAKIRI NA KUAMINI MOYONI MWANGU KUWA WEWE NI MUNGU,
ULIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YANGU, INGIA NDANI YANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA
MAISHA YANGU LEO, AMENI.
Hongera kwa
kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
Na Huduma ya
UKOMBOZI GOSPEL, Arusha Tanzania, Kwa Maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka
wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigospel@gmail.com
Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigospel.blogspot.com
Pia #Like
#Penda Page/Ukurasa wetu au kundi la Fb, ili kupata
habari hizi kwa haraka, zaidi. @ugukombozi Gospel
Pia kwenye mtando
Mpya wakitanzania wa
Pia TAZAMA VIDEO ZETU
HAPA https://www.youtube.com/channel/UCv1tghnugOSpbmb5h6ebJtA (Ukombozi Gospel)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni