Jumamosi, 4 Novemba 2017

NI KESHO UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA, MGENI RASIMI NI EMANUELI SHILATU.

Kava la kitabu cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU
Kava la kitabu cha USFIE JANGWANI na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU
Huduma ya Uandishi wa Vitabu vya Kiroho ya MWALIMU OSCAR SAMBA kesho tarehe 5/11/2017 inatarajia kufanya uzinduzi wa vitabu vyake vipya viwiwli, cha USFIE JANGWANI na kile cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.

Akizungumza na blogu hii Mkurugenzi Mkuu Oscar Samba aliye pia mwandishi wa vitabu hivyo amesema kuwa mgeni rasimi anatarajiwa kuwa ni Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Binafi ya KING DAVID  na pia ni Mkurugenzi  wa huduma ya mafunzo ya mafanikio kiuchumi kupitia Biblia ya KINGDOM BUSINESS.

Afla hiyo ya uzinduzi inatarajiwa kufanyika katika kanisa la TAG VCC Lililopo katika eno la Morombo hapa Mkonia Arusha nchini Tanzania.


Mwalimu na Mkurugenzi Oscar Samba amewalika watu wote kutoka katika dini na kabila zote kuudhuria afla hiyo inayotajiwa kuanza majira ya 9 alasiri hadi 11 jioni.

Huduma hii imeasisiwa na MWALIMU OSCAR SAMBA wa huduma mama ya Ug Ministry yaani Ukombozi Gospel iliyo ya  Ualimu wa Neno la Mungu.

Kitabu cha Usifie Jangwnai kinalenga kuwatia watu moyo kuhusu kusonga mele kiroho na kuwataka kutokukata tamaa maana mafanikio yao yapo katika nchi ya Kanani ila ili kuyapata inawabidi kupitia Jangwani.

Na kile ha Ishi Salama kweye Ndoa Changa kina lengo la kuwataka wanandoa wachanga kutokuishi katika hali ya migogoro sanjari na kuzisaidia ndoa za muda mrefu zenye hali ya Uchanga.

Usikubali kukosa kitabu hiki, kama upo mbali basi fuatilia habari zetu ili ujue mawakala waliokaribu nawe, Mungu akubariki na karibu sana kesho, pia kama unawiwa kuichangi huduma hii kwa fedha zako kwa njia ya M-PESA, fanya hivyo, namba zetu: +255759 859 287.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni