Namna ya Kuishi Salama Maisha ya Uchumba hadi Ndoa.
Kusudio la mada hii ni kukuwezesha kuishi vyema kiroho na kimwili, au kiushuhuda katika maisha ya uchumba.
Swala la ushuhuda ni muhimu sana katika hatua hii maana litawajengea heshima, kwa jamii, jamaa wako wa karibu kiundugu na kanisa kiujumla, kwa hiyo ipo haja ya kuwa salama kiroho na kimtazamo au machoni pa watu pia.
Maana ni vizuri kuhesabiwa haki na Mungu lakini pia wanadamu wakuheshimu. Maana hali hii itakupa haki kwao, lakini pia itaifanya huduma yako kukubalika, maana katika ulimwengu huu tunamuhitaji Mungu kweli ili tufanikiwe, lakini pia tunawahitaji wanadamu, na wanadamu hutazama kwa macho ya kimwili ili kuona, sio ya moyoni na nje kama Mungu.
Maana yangu hapa ni kukutaka kuepukana na mitazamo finyu ya vijana kadha kuwa anaishi kama vile atakavyo yeye madamu hatendi dhambi kwake sio mbaya.
Na kujaribu kutengeneza mazingira ya ushuhuda kwake ni unafiki, huku ni kukosa maarifa.
Hali ya kupita kila kona, au kukaa ovyo na mwenzako ama kukutana katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa mboni za wanadamu, kwa madai kuwa nyie mpo vema kiroho hata kama hamtendi kosa la kukutana kimwili, lakini pia kufanya hivyo ni dhambi.
Inaweza isiwe na madhara au matokeo kama vile ya kujamiiana, ila hali ya kuharibu ushuhuda kwa makusudi ni kosa kiroho.
Paulo Mtume anasema sisi ni barua, licha ya hivyo, anatuambia kama akila nyama itamkwaza jirani yake, yupo tayari kutokuila, unaweza kujione uchaji wa mtumishi huyu ulivyokuwa mkubwa.
Kwa hiyo nawe unawajibika kujiwekea mazingira salama ili jina la Bwana lisitukanwe, hali ya kusema kuwa Mungu anatizama moyo, au ya kuku mayai na ya watu maneno, eti huwezi kuwazuilia kunena, unapaswa kuwa makini ili kumtetea Kristo.
“Madamu sitazini, si dhambi mtumishi.” Acha ujinga, linda ushuhuda.
Huduma nyingi za watu zimekufa, kwa kukosa hii hekima, zimeishilia kupakwa matope na uvundo wa kila namna. Karibu:
(a) Jinsi ya Kutenda Vyema.
(i) Zifahamu Sheria au kanuni za Kanisani kwako, makanisa mbalimbali yametofautia kivigezo, yapo ambayo ili ufunge ndoa au hata uchumba kutangazwa ni lazima, muhusika awe anaudhuria ibada za Ushemasi, Seli, au Jumuia, wenine huziita ibada za Nyumbani, au Kanisa la nyumbani.
Hususani makanisa makubwa huwa na sera hii ili kuweza kuwa na taarifa sahihi za mtu anayenuia kuchukuwa hatua hiyo, kwani kama kanisa lina watu wengi ni vigumu kwa uongozi wa kanisa la mahali pamoja, kujua tabia zake, na kama kweli ana vigezo na sifa za kufikia hatua hiyo, maana wengine huweza kuwa na ndoa nyingine au alishawai kuolewa, na muda wake katika wokovu, na pia hali yake ya kiroho.
Kwa mantiki hiyo, kikundi cha ibada za Jumuia, huweza kukufahamu vizuri zaidi.
Lakini pia wengine, ni shariti uwe umelipa au kutoa Zaka ama fungu la kumi, kwa kipindi kisicho pungua miezi 6.
Pia vigezo vya muda wako wa wokovu au kuabudu hapo kanisani ni muhimu sana.
Kufahamu kanuni na taratibu kama hizo, kutakusaidia kutokuingia katika malumbano ya kihoja na wahusika, pia kutakuokolea muda, licha ya kukuokolea muda kutakufanya kutenda vyema.
Maana nimewaona watu walioabudu makanisani muda wa miaka mingi lakini kwa kuwa walipohamia walihamia kienyeji, yaani bila barua ya utambulisho, walijikuta wakizuiliwa, kuchuku hatua hizi za Uchumba hadi ndoa, na swala lipo sana kwenye huduma zenye watu wengi.
Hatua za Kuchukuwa mkishakubaliana:
(ii) Nendeni kwa Mchungaji, kama mna abudu katika makanisa tofauti tofauti, ni vyema mkaanza katika kanisa la kijana wa kiume, au tumieni utaratibu kwa kila muhusika kumuendea mchungaji wake, na mara baada ya hapo ndipo muwaende walezi wate. Ila kibusara anzeni kwa wakiume.
Ili kulinda ushuhuda mnaweza kuamua kukutana kanisani, ama kutumia utaratibu wa kuambatana na washenga au mshenga.
(iii) Tafuta Mshenga na uambatane nae, ni muhimu kuanza kutafuta mtu huyu maana atafanyika msaada mkubwa kwako, kama utatambua nafasi yake vyema.
Lakini mara baada ya kumpa, huna budi kuhakikisha kuwa unambatana nae, ili kutimiza adhima na dhima ya uwepo wake.
Sifa za Mshenga:
(1) Awe Mchamungu, sifa hii ni muhimu ili aweze kukubeba rohoni, na kukushauri kiroho, lakini pia aweze kukulinda vyema kiroho, pia asije kuhusika katika kukushawishi kuingia majaribuni, pia ili kumrahishia Mungu pale atakapotaka kufikisha jambo fulani kwenu aidha kwa njia ya mashauri na mahusia kutoka kwake.
(2) Awe na uelewa wa kutosha kuhusu Mambo haya, Anapaswa kuyafahamu kwa kiasi fulani maswala ya uchumba, ili aweze kukaa vyema kwenye nafasi yake.
(3) Awe na Uwezo wa Kukushauri na Ujasiri wa Kukukemea, Ajawe na Hekima lakini pia Busara, ili kukusaidia katika kuchukuwa maamuzi fulani, maana kuna majira mambo huweza kuwa magumu kiutatuzi, ila hekima yake na Busara zake huweza kutumika katika kuleta