Leo ninakuletea tu Utangulizi wake, na niyangu rai kukutaka kufuatilia kitabu hiki punde kikiingia Sokoni, pia kwa dhati kabisa ninaomba maombi yako ili nikikamilishe vyema na tena kwa wakati.
Utangulizi:
Kukataliwa maana yake ni kukosa kibali. Hali inayokufanya kukosa mvuto mbele ya wahusika, kutokudhaminika, au kuwa na dhamani ama sifa ama kupata heshima stahiki kutoka kwa jamii inayokukataa ama kukubagua.
Kuna vitu watavifanya bila kukushirikisha angali ulistaili kufanyiwa hivyo, ukisoma kisa kile cha kupakwa mafuta kwa Daudi, utaona kuwa watoto wengine wote waliitwa ila Daudi pekee hakuitwa kwani alisaulika;
1 Samweli 16: 10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Tatizo la kukataliwa huwalinaumiza, linajeruhi, na kumuacha muhisika akiwa katika hali ya unyoge, na kukosa raha, na hali hiyo hiyo ya maumivu ispopata tiba ya haraka huweza kusababisha madhara makubwa mno katika kiroho cha mtu na kimaisha kwa ujumla.
Daudi ni miongoni mwa watumishi walikumbwa na hali au na kadhia hii kwenye Biblia, pia imo kwa Musa, Musa alitaka kuwakomboa wana wa Israeli maana mmoja wao alipoonewa na Mmisiri alihakikisha anamuwa yule muonevu, na alipowaona wao kwa wao wanapigana alijaribu kuwapatanisha, lakini yule muonevu alimgeukia na kuibua hali ya kumkataa Musa kama muamuzi, jambo lililochangia kutoroka au kuikimbia ile nchi, ingawaje sababu nyingine ni hofu kwa Farao, ila na hii ilichangia, maana hakuwa na makazi tena yaliyosalama, kwa Wamisiri Farao anawinda roho yake, na kwa Waebrania wenzake, hawamtaki.
Alhamisi, 14 Desemba 2017
NAFASI YA NVUVU ZA KIROHO KATIKA KUKUTAJIRISHA, KWA WAFANYA BIASHARA NA WASANII. Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha NAFASI YA ULIMWENGU WA ROHO TAKIKA UONGOZI, (kiti cha Enzi)
Mwalimu Oscar Samba na Mtume Doggy Lasi wa nchini Kenya wakiwa katika picha ya Pamoja, Picha na Makitaba yetu. |
.
Kwenye
Biashara:
Biashara inaweza isiingie moja kwa moja katika kundi
la uongozi ila zipo zilizoinuka nakufikia hatua ya kampuni au taasisi fulani ambazo zina mfumo wa
uongozi ndani yake, pia Migahawa na hata Hoteli, Shule na vikundi fulani vya
ujasiriamali na kiuchumi ni miongoni mwavyo.
Lakini hapa ninazungumzia biashara kwa ujumla bila
kujali kubwa au ndogo, maana shuhuli yoyote ile ya kiuchumi inayofanywa na mtu
ni lazima iwe na nguvu ya ulimwengu wa roho.
Ndio maana yapo makabila fulani biashara au kazi
ikienda mrama hupiga simu nyumbani ili warekebishe mambo, pia wengine kila
mwezi fulani hukutanyika nyumbani kwa ajili ya ibada za mizimu, hapo huchinja ama
kufanya mila na wazee kuwaombea dua fulani.
Hilo ni kundi la kwanza, la pili ni lile ambalo kuna
wazee au viongozi wao wa kidini na kuomba dua kutoka kwao, wengine huwapungia
mapepo maalumu ya biashara au kuwaombea kwa mungu ama mzimu wanao uabudu.
Kundi jingine la tatu ni wale wanaoenda kwa waganga wa
kienyeji au wasoma nyota, ama wachawi, ama kufanya ushirikina wowote ule.
Kundi la nne ni wale wanaomuabudu Shetani moja kwa
moja, yaani hawa wanafahamu kabisa kuwa wanamuabudu na kumtumikia Lusifa, dini
yao huitwa ya Mashetani, Kikundi cha “Freemason” na vinginevyo ni miongoni
mwavyo.
Wanachama wake au walio wengi huingia huko ili wapate
fedha, mvuto kwenye usanii kama wana muziki, waigizaji, au kibali kwenye siasa na
kwa bahati mbaya hata viongozi wa kidini nao wamejipenyeza kwenye makundi hayo,
kuna alingine pia wanaliita, “Iluminate.”
Makundi yote hayo niliyoyataja yanatafuta nguvu za
kiroho katika biashara kutoka kwa Shetani, sababu ya wafanya biashara kufanya hivyo
ni kutokana na uhalisia kuwa swala la biashara hufanyika kiroho ama ili kuweza
kufanya biashara mwilini ama kuwa na uwezo wa kumiliki na kutawala kiuchumi ni
lazima uwe na nguvu za ulimwengu wa roho, ambazo hupatika aidha kwa Yesu au
Shetani, sasa wasio na Yesu, hulazimika kutumia njia za mkato. Nakupa andiko
linalodhibitisha jambo hili:
Ufunuo 17-19. (17:4 Na
mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu,
amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe
cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati
wake.
17:5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina
limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.)
Jina lake ni, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA
MACHUKIZO YA NCHI, Ndiye yule anayewapa wanasiasa nguvu ya kutawala, pia
ukisoma kwa umakini Sura ya 17-19 ya Ufunuo utafahamu kuwa maandiko yanasema
kuwa wametajirishwa kwa kiburi chake;
(Ufunuo 18:3
kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali
kwa nguvu za kiburi chake.)
Nakumegea hii siri: Kumbuka hilo andiko linasema kuwa
wafalme, ukiona wafalme fahamu ni wanasiasa au viongozi wa uongozi wa dunia
hii, pia wafanya biashara, alafu wamepata mali au uongozi kwa kiburi chake,
ndio maana mwanasiasa anapoingia madarakani anakuwa na kiburi sana, wapo tayari
watu wauwawe, ila wao waendelee kutawala, wapo tayari kuziona damu za watu wasio
na hatia zikimwagika lakini ulaji wao usipunguke, alikadhalika wafanya biashara,
mara baada ya kuipata mali huingiwa na roho ya kiburi, ukiyaona hayo usishangae
fahamu kiti kinachowawezesha au nguvu inayowanufaisha ama kuwafanikisha ndiyo
inayoachilia hiyo roho ya kiburi, ndipo ninasema kuwa udhamini wa ulimwengu wa roho
unaotoka kwa Yesu una dhamani kubwa sana. (Tusonge
mbele na Biashara)
Jumatatu, 6 Novemba 2017
HUDUMA YA MWALIMU OSCAR VITABU NI JIBU LA KUDUMU KIROHO, KINDOA, KIUCHUMI NA HATA KISIASA NA KIJAMII.
Huduma ya MWALIMU OSCAR VITABU, Imebainisha kuwa imebeba majibu mengi ya maswali na mambo magumu yanayoikabili jamii siku ya leo ikiwemo ile ya Kikristo na isiyo ya Kikirsto.
Hayo yamebainishwa jana (5/11/2017) na Mkurugenzi Mkuu wa huduma hii Mwalimu Oscar Samba wakati akitoa risala kwa mgeni Rasimi katika siku ya Uzinduzi wa vitabu vya USIFIE JANGWNAI na cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.
Mwalimu alielezea maono na malengo ya huduma hii mambo ambayo yanalenga kutoa majibu au kufanyika msaada mkubwa kwa jamii katika utatuzi wa maswala mablimbali yanayoikabili.
Kwa hivi sasa jamii inakabiliwa sana na tatizo la kutokumjua Mungu, kuduma kiroho, Migogoro kwenye ndoa, na hata zile zilizo salama kiamani, nyingi, bado hazitimizi vyema kusudi kuu la kuwekwa kwake na Mungu.
Pia lipo tatizo la kiuchumi, kwani wana wengi wa Mungu wamekuwa wakiishi maisha magumu, pamoja na wale wa dunia hii.
Jambo jingine ni kutokuwa na viongozi sahihi au wenye kuwajibika ipaswavyo, wale wakiroho yaani Watumishi, na wakijamii na serikali yaani wanasiasa.
Pia jamii inakabiliwa na tatizo la uzito kifikra, na hii inatokana na kutokuwepo kwa mahubiri, mafundisho na maarifa yanayolenga kuleta ukombozi.
Mambo yote hayo yamo katika kusudi la huduma hii, nami ninakuletea Maono na Malengo pamoja na Mafaniko, sanjari na Changamoto ya huduma hii kama ilivyoelezwa hapo jana na Mkurugenzi.
Mungu akubariki na kama unahitaji vitavu vyetu tafadhali wasiliana nasi kwa namba nitapakayo kupa punde na pia ukitaka kutoa sadaka yako waweza itoa kupitia hiyo Namba: +255 75 985 9287
Hayo yamebainishwa jana (5/11/2017) na Mkurugenzi Mkuu wa huduma hii Mwalimu Oscar Samba wakati akitoa risala kwa mgeni Rasimi katika siku ya Uzinduzi wa vitabu vya USIFIE JANGWNAI na cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.
Mwalimu alielezea maono na malengo ya huduma hii mambo ambayo yanalenga kutoa majibu au kufanyika msaada mkubwa kwa jamii katika utatuzi wa maswala mablimbali yanayoikabili.
Kwa hivi sasa jamii inakabiliwa sana na tatizo la kutokumjua Mungu, kuduma kiroho, Migogoro kwenye ndoa, na hata zile zilizo salama kiamani, nyingi, bado hazitimizi vyema kusudi kuu la kuwekwa kwake na Mungu.
Pia lipo tatizo la kiuchumi, kwani wana wengi wa Mungu wamekuwa wakiishi maisha magumu, pamoja na wale wa dunia hii.
Jambo jingine ni kutokuwa na viongozi sahihi au wenye kuwajibika ipaswavyo, wale wakiroho yaani Watumishi, na wakijamii na serikali yaani wanasiasa.
Pia jamii inakabiliwa na tatizo la uzito kifikra, na hii inatokana na kutokuwepo kwa mahubiri, mafundisho na maarifa yanayolenga kuleta ukombozi.
Mambo yote hayo yamo katika kusudi la huduma hii, nami ninakuletea Maono na Malengo pamoja na Mafaniko, sanjari na Changamoto ya huduma hii kama ilivyoelezwa hapo jana na Mkurugenzi.
Maono: Kuwa na jamii salama kiroho na
kifikra yenye mafanikio ya kimwili na kiroho katika nyanja muhimu kama ya
kiuchumi, kisiasa, na kuwa huru kiroho katika Kristo Yesu.
Malengo makuu ya Huduma: 1. Kuikomboa
jamii kiroho, kiuchumi, na kisiasa. 2.
Kuzifanya ndoa kuwa sehemu salama, ili kufanikisha kusudi lake vyema. 3. Kuandaa viongozi wazuri na
wawajibikaji kiroho. 4. Kujenga
umoja katika Mwili wa Kristo.
Pia 5. Kuwa na Gazeti la kila wiki, na 6. Kutoa Jarida kila baada ya miezi, 7. Pamoja na kuwa na Press yetu wenyenye
kwa ajili ya kuprinti vitabu. Itakayoitwa, Haleluya
Press.
Mafanikio: 1. Kuandika vitabu Takiribani 24,
ikiwemo 12 vya familia na ndoa, pia vipo vyenye dhima ya kiuongozi kiroho,
mfano cha HEKIMA YA KIUONGOZI KIHUDUMA. Pia 2. Kufanikiwa kuvitoa vitabu viwili
ambavo leo ndio vinazinduliwa.
Changamoto: Ndugu Mgeni Rasimi, zipo changamoto
kadhaa ambazo zinatukabili, hakika zikitatuliwa huduma hii itafanya kazi katika
ufanisi mkubwa sana.
1. Upungufu wa vifaa vya kuandikia na
uchapaji pia uandaaji wa vitabu , tunahitaji Komputa moja ana ya Desktop, yenye dhamani ya shilingi
500, 000/=, kwa ajili ya kuandikia, Printer ya Epsoni yenye dhamani ya sh 650,
000/=.
2. Mtaji kwa ajili ya Kuprinti vitabu, Ndugu mgeni rasimi, huduma hii imeanza
katika nyakati ngumu sana kiuchumi, hadi sasa kazi hii tumeifanya kwa imani
kubwa, hapa tulipo tuna deni la zaidi ya sh 300, 000/=.
Ili kuweza
kufanya kazi hii kwa wakati na ufanisi mkubwa, tunahitaji walau mfuko wetu uwe
na shilingi 600, 000/=.
3. Ukosefu wa Ofisi, Ndugu mgeni Rasimi huduma hii kama
niivyokujuza hapo awali kuwa imeanza kiimani, kwani hadi hivi sasa hatuna ofisi
kwa ajili ya shuhuli zetu, badala yake, nyumbani au chumbani kwa mkurugenzi
Mkuu ndimo ilipo Ofisi, kama unavyojua mazingira ya nyumbani, na matumizi ya
meza ya ofisi yanapoingiliana yale ya nyumbani, hali ambayo sio salama kihuduma
au kiofisi.
Pia swala
hili linazuilia wageni au watu wanao hitaji huduma kuipata kwa urahisi.
4. Ukosefu wa mawakala, Ndugu Mgeni rasimi ni yetu kiu
kutuwezeha kupata mawakala wengi ili kurahisisha swala la usambazaji na uzaji
wa vitabu hivi.
TAZAMA PICHA ZA UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA
Jumamosi, 4 Novemba 2017
NI KESHO UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA, MGENI RASIMI NI EMANUELI SHILATU.
Kava la kitabu cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU |
Kava la kitabu cha USFIE JANGWANI na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU |
Akizungumza na blogu hii Mkurugenzi Mkuu Oscar Samba aliye pia mwandishi wa vitabu hivyo amesema kuwa mgeni rasimi anatarajiwa kuwa ni Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Binafi ya KING DAVID na pia ni Mkurugenzi wa huduma ya mafunzo ya mafanikio kiuchumi kupitia Biblia ya KINGDOM BUSINESS.
Afla hiyo ya uzinduzi inatarajiwa kufanyika katika kanisa la TAG VCC Lililopo katika eno la Morombo hapa Mkonia Arusha nchini Tanzania.
Jumanne, 10 Oktoba 2017
KARIBU KWENYE BLOGU YETU YA HUDUMA YA VITABU VYA MWALIMU OSCAR SAMBA
Pia utajipatia furusa ya kusoma vitabu vya mafundisho, kutia moyo, na vile vya sanaa ya Ushairi.
Mawasiliano:
Simu +255 759 859 287.
Baruapepe: mwalimuoscarvitabu@gmail.com
Pichani ni Mwalimu Oscar Samba aliye Mkurugenzi wa hii huduma. |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)