Alhamisi, 14 Desemba 2017

Kitabu cha NAMNA YA KUTOKA KWENYE KIFUNGO AU HALI YA KUKATALIWA.

Leo ninakuletea tu Utangulizi wake, na niyangu rai kukutaka kufuatilia kitabu hiki punde kikiingia Sokoni, pia kwa dhati kabisa ninaomba maombi yako ili nikikamilishe vyema na tena kwa wakati.
Utangulizi:
Kukataliwa maana yake ni kukosa kibali. Hali inayokufanya kukosa mvuto mbele ya wahusika, kutokudhaminika, au kuwa na dhamani ama sifa ama kupata heshima stahiki kutoka kwa jamii inayokukataa ama kukubagua.
Kuna vitu watavifanya bila kukushirikisha angali ulistaili kufanyiwa hivyo, ukisoma kisa kile cha kupakwa mafuta kwa Daudi, utaona kuwa watoto wengine wote waliitwa ila Daudi pekee hakuitwa kwani alisaulika;
1 Samweli 16: 10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. 
11 Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku. 
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Tatizo la kukataliwa huwalinaumiza, linajeruhi, na kumuacha muhisika akiwa katika hali ya unyoge, na kukosa raha, na hali hiyo hiyo ya maumivu ispopata tiba ya haraka huweza kusababisha madhara makubwa mno katika kiroho cha mtu na kimaisha kwa ujumla.
Daudi ni miongoni mwa watumishi walikumbwa na hali au na kadhia hii kwenye Biblia, pia imo kwa Musa, Musa alitaka kuwakomboa wana wa Israeli maana mmoja wao alipoonewa na Mmisiri alihakikisha anamuwa yule muonevu, na alipowaona wao kwa wao wanapigana alijaribu kuwapatanisha, lakini yule muonevu alimgeukia na kuibua hali ya kumkataa Musa kama muamuzi, jambo lililochangia kutoroka au kuikimbia ile nchi, ingawaje sababu nyingine ni hofu kwa Farao, ila na hii ilichangia, maana hakuwa na makazi tena yaliyosalama, kwa Wamisiri Farao anawinda roho yake, na kwa Waebrania wenzake, hawamtaki.

NAFASI YA NVUVU ZA KIROHO KATIKA KUKUTAJIRISHA, KWA WAFANYA BIASHARA NA WASANII. Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha NAFASI YA ULIMWENGU WA ROHO TAKIKA UONGOZI, (kiti cha Enzi)

Image may contain: 2 people, people standing and suit
Mwalimu Oscar Samba na Mtume Doggy Lasi wa nchini Kenya wakiwa katika picha ya Pamoja, Picha na Makitaba yetu.
.
Kwenye Biashara:
Biashara inaweza isiingie moja kwa moja katika kundi la uongozi ila zipo zilizoinuka nakufikia hatua ya kampuni  au taasisi fulani ambazo zina mfumo wa uongozi ndani yake, pia Migahawa na hata Hoteli, Shule na vikundi fulani vya ujasiriamali na kiuchumi ni miongoni mwavyo.
Lakini hapa ninazungumzia biashara kwa ujumla bila kujali kubwa au ndogo, maana shuhuli yoyote ile ya kiuchumi inayofanywa na mtu ni lazima iwe na nguvu ya ulimwengu wa roho.
Ndio maana yapo makabila fulani biashara au kazi ikienda mrama hupiga simu nyumbani ili warekebishe mambo, pia wengine kila mwezi fulani hukutanyika nyumbani kwa ajili ya ibada za mizimu, hapo huchinja ama kufanya mila na wazee kuwaombea dua fulani.
Hilo ni kundi la kwanza, la pili ni lile ambalo kuna wazee au viongozi wao wa kidini na kuomba dua kutoka kwao, wengine huwapungia mapepo maalumu ya biashara au kuwaombea kwa mungu ama mzimu wanao uabudu.
Kundi jingine la tatu ni wale wanaoenda kwa waganga wa kienyeji au wasoma nyota, ama wachawi, ama kufanya ushirikina wowote ule.
Kundi la nne ni wale wanaomuabudu Shetani moja kwa moja, yaani hawa wanafahamu kabisa kuwa wanamuabudu na kumtumikia Lusifa, dini yao huitwa ya Mashetani, Kikundi cha “Freemason” na vinginevyo ni miongoni mwavyo.
Wanachama wake au walio wengi huingia huko ili wapate fedha, mvuto kwenye usanii kama wana muziki, waigizaji, au kibali kwenye siasa na kwa bahati mbaya hata viongozi wa kidini nao wamejipenyeza kwenye makundi hayo, kuna alingine pia wanaliita, “Iluminate.”
Makundi yote hayo niliyoyataja yanatafuta nguvu za kiroho katika biashara kutoka kwa Shetani, sababu ya wafanya biashara kufanya hivyo ni kutokana na uhalisia kuwa swala la biashara hufanyika kiroho ama ili kuweza kufanya biashara mwilini ama kuwa na uwezo wa kumiliki na kutawala kiuchumi ni lazima uwe na nguvu za ulimwengu wa roho, ambazo hupatika aidha kwa Yesu au Shetani, sasa wasio na Yesu, hulazimika kutumia njia za mkato. Nakupa andiko linalodhibitisha jambo hili:
Ufunuo 17-19. (17:4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

17:5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.)
Jina lake ni, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI, Ndiye yule anayewapa wanasiasa nguvu ya kutawala, pia ukisoma kwa umakini Sura ya 17-19 ya Ufunuo utafahamu kuwa maandiko yanasema kuwa wametajirishwa kwa kiburi chake;
 (Ufunuo 18:3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.)
Nakumegea hii siri: Kumbuka hilo andiko linasema kuwa wafalme, ukiona wafalme fahamu ni wanasiasa au viongozi wa uongozi wa dunia hii, pia wafanya biashara, alafu wamepata mali au uongozi kwa kiburi chake, ndio maana mwanasiasa anapoingia madarakani anakuwa na kiburi sana, wapo tayari watu wauwawe, ila wao waendelee kutawala, wapo tayari kuziona damu za watu wasio na hatia zikimwagika lakini ulaji wao usipunguke, alikadhalika wafanya biashara, mara baada ya kuipata mali huingiwa na roho ya kiburi, ukiyaona hayo usishangae fahamu kiti kinachowawezesha au nguvu inayowanufaisha ama kuwafanikisha ndiyo inayoachilia hiyo roho ya kiburi, ndipo ninasema kuwa udhamini wa ulimwengu wa roho unaotoka kwa Yesu una dhamani kubwa sana. (Tusonge mbele na Biashara)