Hayo yamebainishwa jana (5/11/2017) na Mkurugenzi Mkuu wa huduma hii Mwalimu Oscar Samba wakati akitoa risala kwa mgeni Rasimi katika siku ya Uzinduzi wa vitabu vya USIFIE JANGWNAI na cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA.
Mwalimu alielezea maono na malengo ya huduma hii mambo ambayo yanalenga kutoa majibu au kufanyika msaada mkubwa kwa jamii katika utatuzi wa maswala mablimbali yanayoikabili.
Kwa hivi sasa jamii inakabiliwa sana na tatizo la kutokumjua Mungu, kuduma kiroho, Migogoro kwenye ndoa, na hata zile zilizo salama kiamani, nyingi, bado hazitimizi vyema kusudi kuu la kuwekwa kwake na Mungu.
Pia lipo tatizo la kiuchumi, kwani wana wengi wa Mungu wamekuwa wakiishi maisha magumu, pamoja na wale wa dunia hii.
Jambo jingine ni kutokuwa na viongozi sahihi au wenye kuwajibika ipaswavyo, wale wakiroho yaani Watumishi, na wakijamii na serikali yaani wanasiasa.
Pia jamii inakabiliwa na tatizo la uzito kifikra, na hii inatokana na kutokuwepo kwa mahubiri, mafundisho na maarifa yanayolenga kuleta ukombozi.
Mambo yote hayo yamo katika kusudi la huduma hii, nami ninakuletea Maono na Malengo pamoja na Mafaniko, sanjari na Changamoto ya huduma hii kama ilivyoelezwa hapo jana na Mkurugenzi.
Maono: Kuwa na jamii salama kiroho na
kifikra yenye mafanikio ya kimwili na kiroho katika nyanja muhimu kama ya
kiuchumi, kisiasa, na kuwa huru kiroho katika Kristo Yesu.
Malengo makuu ya Huduma: 1. Kuikomboa
jamii kiroho, kiuchumi, na kisiasa. 2.
Kuzifanya ndoa kuwa sehemu salama, ili kufanikisha kusudi lake vyema. 3. Kuandaa viongozi wazuri na
wawajibikaji kiroho. 4. Kujenga
umoja katika Mwili wa Kristo.
Pia 5. Kuwa na Gazeti la kila wiki, na 6. Kutoa Jarida kila baada ya miezi, 7. Pamoja na kuwa na Press yetu wenyenye
kwa ajili ya kuprinti vitabu. Itakayoitwa, Haleluya
Press.
Mafanikio: 1. Kuandika vitabu Takiribani 24,
ikiwemo 12 vya familia na ndoa, pia vipo vyenye dhima ya kiuongozi kiroho,
mfano cha HEKIMA YA KIUONGOZI KIHUDUMA. Pia 2. Kufanikiwa kuvitoa vitabu viwili
ambavo leo ndio vinazinduliwa.
Changamoto: Ndugu Mgeni Rasimi, zipo changamoto
kadhaa ambazo zinatukabili, hakika zikitatuliwa huduma hii itafanya kazi katika
ufanisi mkubwa sana.
1. Upungufu wa vifaa vya kuandikia na
uchapaji pia uandaaji wa vitabu , tunahitaji Komputa moja ana ya Desktop, yenye dhamani ya shilingi
500, 000/=, kwa ajili ya kuandikia, Printer ya Epsoni yenye dhamani ya sh 650,
000/=.
2. Mtaji kwa ajili ya Kuprinti vitabu, Ndugu mgeni rasimi, huduma hii imeanza
katika nyakati ngumu sana kiuchumi, hadi sasa kazi hii tumeifanya kwa imani
kubwa, hapa tulipo tuna deni la zaidi ya sh 300, 000/=.
Ili kuweza
kufanya kazi hii kwa wakati na ufanisi mkubwa, tunahitaji walau mfuko wetu uwe
na shilingi 600, 000/=.
3. Ukosefu wa Ofisi, Ndugu mgeni Rasimi huduma hii kama
niivyokujuza hapo awali kuwa imeanza kiimani, kwani hadi hivi sasa hatuna ofisi
kwa ajili ya shuhuli zetu, badala yake, nyumbani au chumbani kwa mkurugenzi
Mkuu ndimo ilipo Ofisi, kama unavyojua mazingira ya nyumbani, na matumizi ya
meza ya ofisi yanapoingiliana yale ya nyumbani, hali ambayo sio salama kihuduma
au kiofisi.
Pia swala
hili linazuilia wageni au watu wanao hitaji huduma kuipata kwa urahisi.
4. Ukosefu wa mawakala, Ndugu Mgeni rasimi ni yetu kiu
kutuwezeha kupata mawakala wengi ili kurahisisha swala la usambazaji na uzaji
wa vitabu hivi.